Nenda kwa yaliyomo

Malamata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malamata
Kishungi cha malamata
Kishungi cha malamata
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama jaja)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Manyasi)
Nusufamilia: Panicoideae
Jenasi: Setaria
Spishi: S. verticillata
(L.) P.Beauv.

Malamata (Setaria verticillata) ni spishi ya nyasi katika nusufamilia Panicoideae. Asili ya nyasi hili ni Ulaya lakini sasa imewasilishwa au imesamba katika mabara yote mengine isipokuwa Antakitiki. Ni gugu baya na imeanza kupinga viuamimea. Visuke vina nywele zenye kulabu ndogo zinazorahisisha usambazaji wa mbegu zake kwa manyoya ya wanyama na siku hizi kwa nguo za watu.

Spishi nyingine ya Setaria ni aina ya nafaka: mwele-kichaa (S. italica).

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]