Nenda kwa yaliyomo

Malai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malai jinsi inavyokaa juu ya maziwa yaliyokamuliwa
Krimu iliyopigwa

Malai (pia krimu kutoka Kiingereza: cream), ni mafuta yanayopatikana kiasili katika maziwa ya wanyama. Baada ya kukamua maziwa, malai hukusanyika kwenye uso wa maziwa kama utandu. Utandu huo hutolewa na kukusanywa.

Malai hutumiwa kutengeneza samli, siagi na jibini. Pia katika upishi na kutengeneza vyakula mbalimbali kama aisikrimu.