Makeni
Mandhari

Makeni ni mji nchini Sierra Leone na makao makuu ya Mkoa wa Kaskazini na ya Wilaya ya Bombali. Makeni iko takriban km 120 kaskazini kwa mji mkuu Freetown.
Idadi ya wakazi ni takriban watu 124,634 (kadirio 2015). Mji ulijulikana nchini kwa sababu ya soko lake na msikiti mkubwa. Katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Sierra Leone uliathiriwa vibaya na kuona uharibifu wa nyumba nyingi. Wanamgambo wa upinzani walikuwa na makao makuu yao mjini hapo.
Rais Ernest Bai Koroma alizaliwa mjini.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Makeni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |