Ernest Bai Koroma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ernest Bai Koroma

Ernest Bai Koroma (* 2 Oktoba 1953 Makeni (wilaya ya Bombali) katika kaskazini ya Sierra Leone) amekuwa rais wa Sierra Leone tangu 17 Septemba 2007.

Koroma alikuwa mwanabiashara hadi kujiunga na siasa mwaka 2002 alipokuwa mgombea wa urais wa chama cha All People's Congress dhidi ya rais Ahmad Tejan Kabbah. Akashindwa akaongoza upinzani bungeni. Katika uchaguzi uliofuata wa 2007 alimaliza kama mgombea mwenye kura nyingi. Hakufikia nusu za kura hivyo akasimama tena katika awamu ya pili ya uchaguzi akashinda akaapishwa tar. 17 Septemba kuwa rais mpya.