Majadiliano ya mtumiaji:Yosef
Msumbiji -Mozambik
[hariri chanzo]Bwana Yosef, hujambo? Nakuandikia kuhusu masahihisho yako katika makala ya "Afrika". Umebadilisha marejeo ya "Msumbiji" kuwa "Mozambik". Naomba tuepukane na vita ya uhariri jinsi ilivyo katika wiki nyingine. Kwa yote ninayoelewa jina la nchi kusini ya Tanzania ni "Msumbiji" kwa Kiswahili. Au una habari nyingine? Ningeshukuru ukiniambia.
Halafu kuna tayari makala ya Msumbiji. Ukibadilisha kiungo hakitafikisha kwenye makala. Naomba kabla ya kubadilisha neno tuone kwanza kama kiungo kipo tayari (rangi ya neno kuwa buluu). Kama kipo hatuna budi kubadilisha kiungo pia. Menginevyo tunajenga matata katika kamusi yetu! Lakini tukitaka kubadilisha ni vema kuhakisha kwa kamusi kama mwenzetu labda alikuwa na sababu nzuri za kuandika jinsi alivyoandika. Kam kuna wasiwasi basi tuandike kwanza katika ukurasa wa majadiliano tutaje sababu zetu halafu tusubiri siku mbili. --Kipala 17:03, 20 Aprili 2006 (UTC)
Asante kwa jibu. Tukiandikiana ni bila samahani. Kila moja ana mchango wake, tusipokubaliana tujadiliane. Basi. Kuhusu Ethiopia: Uhabeshi ni kawaida pamoja na Ethiopia. Muhimu tu kuweka viungo. Kompyuta pekee yake haiwezi kuunganisha lazima tufanye sisi. Kwa mfano ukiandika "Uhebeshi" hupati kitu. Ukiandika "Uhabeshi" unafikishwa Ethiopia. --Kipala 20:00, 20 Aprili 2006 (UTC)
- Kipala amesema kweli. Mfumo hii inaitwa "redirection" kwa Kiingereza. Kwa mfano, hivi karibuni niliunda redirect mpya, kutoka Mozambiki mpaka Msumbiji. Sasa majina yote mawili yanampekelea mtu kufika makala moja. Niliandika (katika Mozambiki):
- #REDIRECT [[Msumbiji]]
- Ukijua kiingereza, en:Wikipedia:Redirect makala hii ina maelezo zaidi. Matt Crypto 23:51, 20 Aprili 2006 (UTC)
Majadiliano
[hariri chanzo]Hujambo Yosef, na karibu Wikipedia! Ninakushukuru kwa michango yako ya mwezi huu. Nina mapendekezo mawili: ungependa kuzumgumza na mtumiaji mwingine, utumie ukurasa wa majadiliano. Kwa mfano, User talk:Kipala badala ya User:Kipala. Pia, unaweza kutia saini baada ya ujumbe wako kwa kutumia "tilde" nne mfululizo, yaani ~~~~. Programu ya Wikipedia itabadilisha hii kwa jina lako na tarehe. Matt Crypto 15:13, 21 Aprili 2006 (UTC)
Kuendeleza wikipedia
[hariri chanzo]Yosef, asante kwa swali. Hapana mimi si mratibu wala msimamizi wa wikipedia bali mwandishi mwenzako tu. Ni kweli ya kwamba tuko wachache sana. Hata katika wikipedia tunapambana na umaskini wa Afrika na urithi wa ukoloni. Umaskini umesababisha uhaba wa kompyuta na wenye kompyuta katika Afrika. Ukoloni umesababisha ya kwamba Waafrika wengi wasomi hawajiamini katika utamaduni wao; Waafrika wa Mashariki wengi awajui Kiswahili vizuri. Hata wasomi Watanzania wengi wanajieleza vizuri zaidi kwa Kiingereza kuhusu utaalamu fulani. Tokeo ni ya kwamba idadi yetu bado ni ndogo, asilimia kubwa kwetu ni ama Waafrika wanaokaa nje ya Afrika au watu wa nje (kama mimi) wapenda wa Kiswahili. Kwa upande mwingine wikipedia ina nafasi kubwa sana hasa katika mazingira ya Afrika. Kwa sababu za kiuchumi siamini ya kwamba kamusi itapatikana karibuni kwa Kiswahili. Lakini idadi ya vijana wanaotumia compyuta kwa njia ya mgahawa wa mtandao (internet cafe) inakua.
Naona tuendelee kuandika na kujenga wikipedia. Kila mmoja anayejiunga ni hatua mbele! Kama wewe unaona wito la kuangalia jiografia basi vizuri! Angalia masanduku ambazo nilitafsiri mimi au sanduku aliyoandaliwa na Matt halafu endelea! Kama una swali nitafurahi kutoa ushauri. --Kipala 17:08, 21 Aprili 2006 (UTC)
Mchapa kazi
[hariri chanzo]Nataka tu kusema Hongera kwa mchapa kazi!! Bwana unasukuma siku hizi. Safi! Sipendi kukuchelewesha lakini ukipata nafasi labda ujaribu kuangalia kidogo tahajia (namna ya kuandika maneno) - itasaidia viungo. Lakini hata hivyo: kitu kikubwa ni uendelee kuweka misingi - hata kama wengine wananyosha baadaye! --Kipala 18:37, 26 Aprili 2006 (UTC)
Kwa kutumia Infobox
[hariri chanzo]Yosef, kama Kipala ameshasema, umefanya kazi kwa bidii! Ninapendekeza tutumie mbinu inayofuata hunakili Infobox ya nchi ("Sanduku la habari ya nchi") kutoka Wikipedia ya Kiingereza ("en" kwa mfupi) mpaka hapa ("sw"). 1) Unakili "wikicode" za infobox ya makala ya en, na ziingize hapa sw. 2) Ubadili vitu vya kulia tu, vitu baada ya alama ya "=". Lakini kabla ya "=", usibadili. Kwa mfano, ikiwa mstari mmoja kutoka en ni:
- conventional_long_name = Republic of Angola |
Ubadili kwa:
- conventional_long_name = Jamhuri ya Angola |
Na kadhalika. Mfano kamili ni, k.m. hapa.
Manufaa ya mbinu hii ni kwamba ni rahisi kunakili Infobox kutoka en mpaka sw bila kazi mno. Isitoshe, nitatengeneza programu ya tarakilishi ya kikaragosi kubadili vitu kama conventional_long_name kwa jina_la_kawaida k.m. baada ya binadamu amenakili. Matt Crypto 19:31, 26 Aprili 2006 (UTC)
Aulakogenia
[hariri chanzo]Yosef, habari - nimeona umeandika kwenye makala kuhusu Aulakogenia. Labda unaweza kutafakari kulinganisha makala na makala yaliyopo kuhusu "gandunia", bamba la gandunia, na kadhalika. Tuelewane tutumie maneno gani. Unaonaje? --Kipala 16:32, 13 Desemba 2006 (UTC)