Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya mtumiaji:Rberetta

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Salamu Rberetta, nimefurahi sana kuona masahihisho yako ya mara kwa mara. Unafanya kazi ya maana sana ninatumaini utakaa nasi na kuendelea! Nikiangalia michango yangu mwenyewe ni kweli mimi si fundi sana kusoma tena yale niliyoandika kwa hiyo makosa ya typo yanabaki mno - pia tuna wachangiaji wengi kidogo wasiozoea kuandika Kiswahili safi. Karibu sana!! Kipala (majadiliano) 19:42, 14 Oktoba 2014 (UTC)[jibu]

Asante kwa maneno yako mema. Ninafurahi kujua kwamba unaziangalia kidogo kazi zangu, kwa sababu ninaogopa nitafanya makosa pia! Kusema kweli, ninaweza kukagua maandiko kwa makini kwa sababu mimi ni mwanafunzi tu, na nasoma polepole sana. Lazima nisome kila herufi, kwani nikisoma upesi sitakuwa na uhakika kusoma kwa usahihi.

Kipala, ukijua kurasa maalumu kwamba ungependa kuhaririwa, tafadhali niambie kuhusu hizo. Nipo radhi kufanya kazi unayopendekeza.

Upangaji wa kurasa za Punda, Punda-Kaya, na Asinus

[hariri chanzo]

Umeona jibu langu katika majadiliano yangu?
Rberetta salaam. Umefahamu vizuri lakini hakuna haja kuomba samahani. Ulifanya vile ulifikiri ni bora. Lakini tunapendelea kurasa zenye vichwa kwa Kiswahili. Endelea kazi yako nzuri. ChriKo (majadiliano) 21:42, 27 Oktoba 2014 (UTC)[jibu]

Ndiyo, niliona jibu lako - asante! Nimeendelea kupitia kurasa za wanyama ulizoanzisha, na sasa ninaelewa vizuri zaidi muundo unaotumia. Rberetta (majadiliano) 22:08, 27 Oktoba 2014 (UTC)[jibu]
We Babu salaam na karibu katika Wikipedia ya Kiswahili. Awali nilidhani wale watu wa buu-baa, kumbe ni mtalaamu na mwandishi mzuri wa Kiswahili. Ninakukaribisha kwa mikono miwili ili tuendeleze gurudumu hili la Kiswahili. Salaam nyingi kutoka mjini Dar es Salaam, Tanzania. Niite Muddyb au,--MwanaharakatiLonga 03:33, 30 Oktoba 2014 (UTC)[jibu]
Salamu Muddyb - asante kwa maneno yako ya kukaribisha! Lakini, kwani mimi ni mwanafunzi wa Kiswahili tu, naona umenipa fumbo zuri - maana ya "buu-baa". Naomba unitaalamishe!  :) Rberetta (majadiliano) 15:06, 30 Oktoba 2014 (UTC)[jibu]
Salaam. Pole kwa kimya kingi. Haya, buu-baa = hit and run! Yaani, hivi umekuja mara-moja tu kutuvuruga kisha mbio. Kumbe, nia yako ni tofauti kabisaa. Uniwie radhi kwa dhana potofu + ukimya wangu. Wako kijana mtiifu, Muddyb au,--MwanaharakatiLonga 11:16, 4 Novemba 2014 (UTC)[jibu]


Kuhusu mkutano wa Machi 2015 na mawasiliano na WMF

[hariri chanzo]

Salaam naomba utazame hapa: Majadiliano_ya_Wikipedia:Wakabidhi#Mawasiliano_na_ofisi_ya_WMF_-_Wikimedia_Foundation_.2F_Asaf_Bartov na kuchangia. Kipala (majadiliano) 09:56, 3 Desemba 2014 (UTC)[jibu]

Kipala salaam. Hukukosea - niko mbali Marekani, na siwezi kuja Tanzania tena mwaka ujao. Lakini, ningependa kufuata vitendo vya mkutano - natumaini taarifa za mkutano zitachapishwa. Pia, labda nitakuwa na dhana ambayo mngependa kusikia. Je, nikikuandikia maelezo ya dhana yangu, labda utaweza kuizingatia, na kuitoa mkutanoni ukifikiri inastahiki? Rberetta (majadiliano) 17:28, 3 Desemba 2014 (UTC)[jibu]

Kazi ya kufanya

[hariri chanzo]

Rberetta salaam. Tunafurahi sana kwamba umeanzisha kurasa kuhusu mamalia. Ni kweli, bado hakuna kurasa nyingi kuhusu wanyama wasiotokea Afrika. Lakini, isipokuwa wanyama wanaojulikana sana, nafikiri hiyo si kipaumbele. Ningependa unisaidie kumaliza kurasa kuhusu wanyama wa Afrika na kuandika nyingine mpya. Waafrika waelewe wanyama wao kwanza (siku hizi wengi hawajui majina kwa lugha zao wenyewe). Kwa sasa mimi ninashughulikia kurasa kuhusu arithropodi. Ukikubali nitakushukuru sana. ChriKo (majadiliano) 15:24, 7 Desemba 2014 (UTC)[jibu]

Ndiyo ChriKo, nipo tayari kukusaidia na kazi yako, lakini ningependa kuendelea na nia yangu pia! Labda asilimia 50/50?

Kwanza, kuhusu kazi yako: Mimi sina ujuzi wa wanyama wa arithropodi kamwe, hata istilahi ya sehemu za miili yao kwa Kiingereza sijui! Lakini, ukitaka nifanye kazi kutafsiri kurasa za arithropodi kutoka Kiingereza, ninafurahi kujaribu kufanya hivyo. Baada ya mimi kumaliza tafsiri, lazima uangalie kazi yangu na kufanya maharirio. Kwa hivyo nitajifunza na kuendelea kuboresha Kiswahili changu. Badala yake, ningeweza kutafsiri kurasa za mamalia ambazo sasa ni mbegu. Bado ningeomba uangalie kazi yangu. Ukiwa na kurasa mahususi ambazo ungependa niziangalie kutafsiri, au kazi nyingine, tafadhali niambie.

Kuhusa nia yangu, tafadhali nipe nafasi kueleza. Zingatia wanafunzi wanaovutiwa na biolojia. Labda wameona mfumo wa uainishaji wa kibiolojia, na wanastaajabu sana. Mimi ninasikitika kidogo kwamba hao wanafunzi watavumbua mti wa uainishaji (kwa Kiswahili tu), na wataona kwamba matawi mengi yapo matupu katika Wikipedia. Kwa hiyo, nia yangu ni kuanzisha ukurasa mmoja tu katika kila jenasi iliyo tupu sasa hivi. Najua tuna shida za kuchagua majina, na labda kuna wachache wanaojali kuhusu wanyama hawa, hasa ambao hawawezi kusoma lugha nyingine, lakini nina hamasa kuwasaidia hata wachache.

Pia, nia yangu ni kuleta Vigezo vingine vya oda za mamalia ambavyo havijatafsiriwa bado, kama Kigezo:Carnivora, na kufanya kawaida kurasa nyingi na kuboresha upangaji wao. Wewe na wengine wa jamii mmefanya kazi nyingi sana hapa, lakini vitu vingi vinahitaji uhariri, na nafikiri mimi ndiye mhariri mzuri kuliko mwandishi. Rberetta (majadiliano) 19:58, 7 Desemba 2014 (UTC)[jibu]

Salaam. Inaonekana kama sikueleza vizuri. Sikuulizi kumaliza au kuandika kurasa za arithropodi. Nitaendelea kazi hii. Tafadhali shughulikia kurasa za mamalia na ndege. Kuhusu kazi yako binafsi, andika kwanza kurasa za makundi makubwa (oda, familia za juu, familia, nusufamilia). Kufanya kila jenasi ni kazi kubwa mno. Kutengeneza vigezo vipya ni mpango mzuri. ChriKo (majadiliano) 21:57, 7 Desemba 2014 (UTC)[jibu]
Pole - sikusoma vizuri mara ya kwanza. Nitafanya kama ulivyouliza. Nitachagua kurasa za wanyama zilizo mbegu sasa, na zilizo na kurasa za Kiingereza zinazolingana nazo, na nitakuonyesha machaguo yangu kabla ya kuanza kazi. Shida ndogo ni kwamba ninahitaji kurasa za Kiingereza kutumia kama chanzo cha kutafsiri. Kurasa za oda au familia huandikwa kama makala ya kisayansi, kwa kawaida, na mimi siwezi kuzitafsiri vizuri. Kwa hiyo, nitachagua kurasa zilizo na kurasa rahisi za Kiingereza zinazolingana nazo. Rberetta (majadiliano) 23:46, 7 Desemba 2014 (UTC)[jibu]
Asante Rberetta. Kila msaada utathaminiwa. Na nitakusaidia ikiwa lazima. Uliza tu. ChriKo (majadiliano) 22:32, 9 Desemba 2014 (UTC)[jibu]

Tafadhali uangalie jamii kuhusu mfumo wa kuanzisha makala

[hariri chanzo]

Mpendwa, nakuomba kuaangalia ukurasa wa Jumuiya. Tuliomba wikimedia ya kutpa mfumo wa kuzuia watumiaji wasiojiandikisha wasianzise makala mapya. Kusudi lilikuwa kupunguza idadi ya makala mabaya yasiyotosheleza masharti ya wikipedia ilhali tuko wachache mno kuziangalia. Wikipedia kubwa kadhaa zinatumia utaratibu huu (kama en:wikipedia) lakini sisi tunapaswa kupeleka ombi kwa kamati fulani. Kamati hii wametupa nafasi kwa kipindi ha miezi 6 tu inayokwisha karibuni. Sasa wanakamati wamekuja wanadai tujieleza au watarudisha mfumo huu nyuma. Mimi nikiwa 1 kati ya wachache wanaochugulia makala mapya naona itaturudisha nyuma. Naomba mchangie! Sanaaaaa!! Kipala (majadiliano) 23:40, 10 Septemba 2015 (UTC)[jibu]