Majadiliano ya mtumiaji:Nairobi123

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Karibu Ndugu Nairobi123 katika Wikipedia ya Kiswahili. Ni furaha yetu kuona tunapata wachangiaji wapya. Iwapo una swali lolote, tafadhali jisikie huru kuuliza! Haya, nimeona umefanya makala kadha wa kadha. Ni hatua nzuri, lakini kasoro ndogondogo ambazo muda si mrefu utakuwa na uwezo wa kuzimaliza. Niite Muddyb, au,--MwanaharakatiLonga 09:37, 19 Julai 2013 (UTC)

Ndugu Nairobi123, asante kwa hariri zako kwenye ukurasa wa lango Kenya! KAzi nzuri! Kipala (majadiliano) 07:18, 1 Aprili 2015 (UTC)
Naam, mzee Kipala. Anahitaji msaada kiduchu! Ngoja nione nini nitafanya!--MwanaharakatiLonga 15:53, 1 Aprili 2015 (UTC)

Muundo na Kigezo la Habari za Nchi[hariri chanzo]

Ni aje waandishi wa Wikipedia ya Kiswahili hawawezi kuelewa ya kwamba tunafaa kuimarisha Kiswahili yenyewe na lugha za Kiafrika. Sifichi ya kwamba lugha rasmi ya hizi nchi ni Kiingereza, Kifaransa na kadhalika lakini ni nani huyo hajui jina la Kenya ya kirasmi ni republic of Kenya, na pia kama haujui unaweza pata hiyo jina kwenye article za Kiingereza, hapa tuko kwenye Wikipedia ya Kiswahili. Nakubaliana nawe huu ni uwanja wa elimu kwenye articles za kiamhara watu wanaelewa jina rasmi kwa lugha yenyewe. Hapa articles mingi hazina jina rasmi ya Kiswahili, infobox zenyewe zikona makosa mengi na hazina habari kuhusu vitu muhimu kama uchumi na kadhalika (nilikuwa naanziana pole pole na nchi kadhaa halafu ningeendelea kuongeza habari muhimu pia pole pole nikiendelea na nilikuwa nataka kutumia format moja ya nchi zote za Kiafrika). Kuhusu mambo ya South Sudan Oyee! angalia article ya Sudan Kusini kwa Kikorea (inaaitwa 남수단 kwa Kikorea) wametafsiri hadi Wimbo wa Taifa iwe (남수단 만세!) kwa lugha ya Kikorea. Hawajaweka jina la wimbo wa taifa kwa Kiingereza wameitafsiri papo hapo kwa sababu ni Wakorea watasoma hiyo article sio watu ambao wanaongea Kiingereza. Kwa hivyo mabadilisho yangu yote yamefanywa nikifananisha article za lugha zingine na pia nikitaka kusisitiza elimu ya lugha ya Kiswahili. Sijaifanya bila kufikiria na kufananisha kama vile unavyofikiria. Niliangalia mifano mbali mbali nikaamua misanduku yote iwe na format moja ambayo inaonyesha vitu kwa Kiswahili. Kwa hivyo muundo unafaa kubadilika kabisa. --Nairobi123 (majadiliano) 8:38, 22 Mei 2020 (UTC)

Ni kweli masanduku yako tofauti, mengine ni ya zamani, na mengine yana taarifa zilizopitwa na wakati. Lakini kwa suala la majina na lugha naungana na Kipala. Kwanza tukubaliane kuhusu sanduku tunalotaka kulitumia, moja kwa nchi zote, walau za Afrika. Halafu ufanye kazi ya kuyabadilisha ili yafanane na yawe na taarifa ya kisasa. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:46, 22 Mei 2020 (UTC)
Nakubali hali ya masanduku hairidhishi sana. Wakati wa kutunga makala mara nyingi tumenakili jedwali la Kiingereza; hapa tumepata fomati tofauti, mara kutoka enwiki, mara kutoka simplewiki, mara nyingi vigezo (templates). Pia vigezo hivi vimebadilishwa katika mwendo wa miaka pale kwenye asili. Tena sehemu ya vigezo hazikutafsiriwa bado. Rafiki Nairobi123 anatunga kila kitu kipekee bila kigezo, sivyo? Sitaki kupinga lakini njia ya kigezo inawasaidia wachangiaji wapya kuingia, ila tu heri tuwe na vigezo vichache au kimoja tu. Na tujitahidi tutafsiri sehemu zake zote (vigezo vidogo - subtemplates). Je Nairobi123, unaona kama unaweza kutunga kigezo? Kipala (majadiliano) 09:01, 22 Mei 2020 (UTC)
Sawa sawa. Nimeanza kuangalia vigezo za wikipedia kwa lugha zingine. Na nataka kutunga kigezo lakini itakuwa kazi mingi na itachukua muda mrefu. Baada ya kurudi chuo kikuu nimekuwa na kazi mingi, sana sana kwa maabara. Huku shuleni sisi hufanya mararibio (experiments) kwa hivyo lazima tuandike ripoti na kadhalika. Kwa hivyo mimi huandika articles hapa mara kwa mara hapo awali nilikuwa nachangia zaidi. Kigezo cha Kiswahili cha habari za nchi iko hapa Kigezo:Sanduku la habari za nchi. Ya kiingereza iko hapa en:Template: Infobox country. Lugha ingine ambayo naweza elewa ni Kikorea kigezo iko hapa ko:틀:나라 정보. Kwa maoni yangu tunafaa kuwa na kigezo ya ambayo imefikia hizo kiwango ndio wachangiaji wapya waweze kuandika. Na pia kigezo lazima isitokee na errors kama vile msanduku wa Kenya ulikuwa unakaa. Nitajaribu kupata wakati wa kuandika kigezo na nitakutumia ujumbe nikianzana nayo. --Nairobi123 (majadiliano) 5:44, 23 Mei 2020 (UTC)
Kadri ya muda nilio nao naweza kusaidia. Labda useme ni habari gani unazopenda kuongeza katika kigezo hiki. Na unaona kasoro wapi. Kipala (majadiliano) 09:52, 23 Mei 2020 (UTC)
Nimekuwa nikifuata mjadala huu. Ili kuunda kigezo haraka, ni rahisi kunakili code kutoka chanzo cha kigezo unachotaka. Kile unachoona kikiwa na muundo unaokufaa. Kisha uhariri ukitumia lugha ya Kiswahili. Kama nilivyofanya na Infobox ya Kaunti za Kenya.
Kimsingi ni sawa. Nimefanya hivyo mara nyingi. Lakini vigezo vingi vimekuwa tata, yaani kuna kigezo ndani ya kigezo, na ndani ya kigezo cha kwanza tena vigezo vingine. Hii ni sababu vigezo vikubwa kwenye enwiki hulindwa, ni wachache tu wenye kibali cha kuhariri, visiharibiwe. Hapa iko changamoto. Yote yanawezekana, lakini ni kazi ya hatua kwa hatua.... (na kama umeshachoka mwishowe unaingiza kigezo kinachotafsiri kilomita zote kuwa maili, hali ambayo hatuhitaji na hatutaki) Kipala (majadiliano) 15:18, 23 Mei 2020 (UTC)