Majadiliano:Umbra
Mandhari
"umbra", "kitovu cha kivuli" au "kivuli kamili"
[hariri chanzo]Mambo? Nimeona kwamba makala mbalimbali zinatumia istilahi mbalimbali. Makala hii inatumia "umbra" na "penumbra" (kutokana moja kwa moja na Kiingereza). Makala ya kivuli inatumia "kivuli kamili" na "nusu kivuli". Makala za kupatwa kwa mwezi na kupatwa kwa jua zinatumia "kitovu cha kivuli" na "kivuli cha kando". Tuchague istihali moja tu.
Kwa maoni yangu "kivuli kamili" na "nusu kivuli" ni bora. Istilahi hii imekwishatumiwa kwenye makala ya kivuli. Kisare (majadiliano) 07:15, 27 Oktoba 2024 (UTC)
- Kwanza nakushukuru kwa kutushirikisha. Pili, baadhi ya istilahi zilijadiliwa katika warsha maalumu kati ya wanawikipedia, wanaastronomia na wanaisimu wa TUKI. Mimi nilihudhuria nusu tu, hivyo sijui zaidi. Nakumbuka tulibuni neno paoneaanga. Kuhusu umbra siwezi kusema makubaliano yalikuwaje. Ila neno kivuli linatumika pia kwa maana ya fotocopy. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:26, 27 Oktoba 2024 (UTC)