Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Ubatizo

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

sidhani kuwa watu waliamuliwa kuwabatiza watotot wadogo bali watakao amini nao wabatizwe ila watoto wadogo hawaelewi lolote juu ya kuamini.....

siku ya kuabudu

[hariri chanzo]

je siku ya kuabudu ni ipi?

Kila siku, mpendwa. na kila saa. Hasahasa kwa watu wa Agano la Kwanza siku ya kukumbukua kukamilishwa kwa uumbaji wa dunia (siku ya saba= Sabato= Jumamosi), kwa watu wa Agano la Pili ni siku ya kufufuka kwa Yesu (=siku ya kwanza Jumapili). Kwa ndugu Waislamu ni siku ya Ijumaa, Kwa wengine siku zisisorudia katika mfumo wa wiki. - Na wewe usisahau kujiandikisha na kutia sahihi! --Kipala (majadiliano) 16:05, 27 Mei 2015 (UTC)[jibu]

Kuhusu ubatizo..

[hariri chanzo]

kwanza ningependa kuwa watu wote waelewe mambo yafuatayo., >>Je, nini maana ya Neno ubatizo? >>Je, ubatizo ulianzia wapi? >>Je, kwa nini tubatizwe?

   Pamoja na kuyaweka maswali hayo, hapo, naomba niseme tu kwamba, hakuna ubatizo wa watoto wachanga, Bali ubatizo ulipo ni ubatizo wa maji mengi tu, 
   Tunapomchukua YESU mwenyewe aliye kielelezo chetu, tunapata kuona katika maisha yake jinsi alivyo batizwa katika MTO yordani kwa kuzamishwa , na kielelezo hicho tukaachiwa na yeye mwenyewe,..
    Mitume wanapokuja kubatiza, kielelezo wanachokifuata ni cha YESU mwenyewe, na sio cha mwingine. Ingawa dhehebu la kikatoliki limekuwa na madai tofauti, kuhusu ubatizo, madai hayo si sahihi, kwa sababu hayatokani na NENO na Mungu..
 Madai yao haswa kwa yule stefana aliyebatizwa pamoja na nyumba yake yote, sio kweli kwamba ni mpaka watoto walibatizwa, bali anaposema kwamba watu wa nyumba yake yote, maana yake ni wale ambao walio kuwa wameshasikia injili kutokana na mahubiri ya Paulo na sila... Na kumbuka kuwa hata kama nyumba hiyo ingelikuwa na watoto, wasingeliweza kubatizwa kwa sababu hakuna Agizo la ubatizo, lililokuwa limeachwa na YESU juu ya watoto wachanga.. Bali yeye mwenyewe aliwaambia kwamba yule aaminiye na kubatizwa ndiye ambaye angeokoka, na ambaye angekataa angehukumiwa, sasa tunaporudi kwa mtoto mchanga, hawezi kufanya maamuzi kama hayo, kwa kuwa ufahamu wake juu ya mambo ya ubatizo haujui  chochote , ..
  Lazima pia tujue kwamba Neno la MUNGU huwa halijipingi.

Hivyo elimu ya Ubatizo wa watoto wachanga ni mapokeo ya watu tena wasio mjua MUNGU. Yuda Aloyce Mwacha. (majadiliano) 19:55, 10 Novemba 2017 (UTC)[jibu]

Asante kwa maoni hayo, lakini acha nikuambie kwamba hujajua vizuri mambo mengi.

1) Yesu alibatizwa na Yohane ubatizo wa maji tu, kumbe mwenyewe alianzisha ubatizo wa Roho Mtakatifu na moto: ni tofauti sana, alivyoeleza Yohane. 2) Yohane alibatiza katika mto Yordani, asibanduke nao kwa sababu alihitaji maji mengi; kumbe Yesu ametutuma kwenda mahali pote kubatiza watu wote, hata wale wa jangwani. 3) Mitume hawakufuata mfano wa Yohane, bali walibatiza katika mazingira yoyote: soma Matendo yao toka mwanzo hata mwisho: utaona karibu wote walibatizwa katika mazingira ya maji machache (isipokuwa akina Lidia huko Filipi). Paulo mwenyewe alibatizwa ndani ya nyumba, kwa kuagizwa, "Simama ubatizwe". 4) Ubatizo wa watoto wachanga upo toka mwanzo wa Kanisa, lakini wa kwanza kuupinga walitokea zaidi ya miaka 1,000 baadaye huko Ulaya, baada ya mazingira kubadilika. 5) Mitume walikuwa Wayahudi waliozoea ibada ya tohara siku ya nane baada ya kutahiriwa iliyomuingiza mtoto katika dini yao. Hivyo wasingeona ubaya wa kuingiza watoto katika Ukristo pia. 6) Tena Wayahudi walipopokea watu wa mataifa walioamini dni yao, kabla ya kuwatahiri wanaume na watoto wao wa kiume walikuwa wakiwamwagia maji wanafamilia wote. 7) Kwa vyovyote ubatizo wa watoto wachanga upo, unafanyika katika madhehebu yaliyo mengi. Labda useme tu kwamba baadhi yanaukataa. Naomba uchunguze hayo ili kujua ukweli, usimlazimishe Mungu kusema ulichowaza wewe. Yeye akupe amani! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:32, 11 Novemba 2017 (UTC)[jibu]