Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Silent Ocean Tanzania

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makala ama ibadilishwe au kufutwa. Habari zake si sahihi. Hii ni kampuni ya Kichina (si ya Kitanzania), tena siwezi kukuta taarifa juu yake. Vyanzo vyote ni vya wenyewe. Tovuti yao ina Kiingereza kibaya kiasi kwamba makala inarudia nukuu kuwa kampuni hii "inasafirisha karibu asilimia tisini ya vifaa kote ulimwenguni" ambayo si kweli hata kidogo. Hapa iko swali la umaarufu. wanfanyakazi 2000 kwa kampuni ya kimataifa si namba kubwa kweli. Sijui kama hii ni jaribio la kutangaza kampuni au makala tu ambayo mada yke haikuchunguliwa. Kipala (majadiliano) 08:14, 2 Septemba 2020 (UTC)[jibu]

Bado naona heri makala ifutwe. Nikiangalia tanbihi, hazithebitishi habari ndani ya makala. Kufuatana na chanzo 2, "Silent Ocean Limited is a clearing & Forwarding company based in Guangzhou, China". Kwa hiyo si kampuni ya Kitanzania jinsi inavyodaiwa. Inawezekana kuna tawi la kampuni ya China katika Tanzania iliyoandikishwa pale pia. Idadi ya wafanyakazi haina uthebitisho, kinyume cha maelezo ya makala. Uhusiano na Samakiba Foundation hauna uthibitisho. Tatizo kubwa ni matumizi ya marejeo ambayo hayathibitishi habari ndani ya makala. Je hii ni kusudi au dalili ya kutoelewa vyanzo? Makala ina harufu ya kupigia debe kampuni, basi ni kinyume cha utaratibu wetu. Kosa kuu ni: hakuna vyanzo visivyo vya wenyewe. Lemma hii imeshafutwa kwenye enwiki kama spam, tazama en:User_talk:Molee4real, na pia pale matumizi ya marejo yalikosolewa ambayo hayalingani na habari za makala. Kipala (majadiliano) 08:29, 14 Septemba 2020 (UTC)[jibu]
Makala imejikita sana kama maelezo ya kibiashara, hivyo naona ifutwe.Czeus25 Masele (majadiliano) 09:55, 14 Septemba 2020 (UTC)[jibu]
Ni vema kupeleka mawazo kuhusu swali la kufuta pia kwenye ukurasa wake, [[1]]. Azimio litatokea pale. Kipala (majadiliano) 10:58, 14 Septemba 2020 (UTC)[jibu]