Majadiliano:Shabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Maelezo?[hariri chanzo]

Shabu kwa hakika si alumini. Labda ni en:alum kwa jumla, labda inamaanisha en:Aluminium sulfate (ling. https://www.jamiiforums.com/threads/shabu.181477/). Katika tovuti nyingine naona ya kwamba "shabu" inamaanisha kampaundi ya iodini ("nilifundishwa kuweka "Iodine pellets" ndani ya mkoba wangu kama kinga ya kunywa maji yoyote mbele yangu kwa kuwa tulitembea siku nane usiku na mchana ndio kikaeleweka. Iodine pellets kwa kiswahili ni "shabu" tena zipo tele masokoni na pengine madukani." - http://afya2012.blogspot.de/2013/01/maji-ni-uhai.html), ila tu iodoni si nyeupe. Je inawezekana neno hili linatumiwa kwa madawa mbalimbali?? Naomba mchangiaji anayeelewa maana nini asahihishe makala; haiwezi kubaki bila kutaja vyanzo. Kipala (majadiliano) 17:01, 11 Septemba 2017 (UTC)

Basi naona kwa Sacleux Shabu ni en:alum, nasahihisha ipasavyo. Kipala (majadiliano) 18:42, 11 Septemba 2017 (UTC)

Inaonekana ukurasa unaohusika zaidi kwa Kiingereza ni Potassium alum. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:55, 12 Septemba 2017 (UTC)