Nenda kwa yaliyomo

Shabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shabu (kwa Kiingereza "alum") ni kampaundi ya kikemia inayounganisha alumini, kali, sulfuri na oksijeni na fomula yake ni KAl(SO4)2. Inatokea kiasili kama madini ambayo yanachimbwa ardhini, yana rangi nyeupe kama chumvi au chokaa.

Shabu ilianza kugundulika tangu kale na kutumiwa kwa kutia rangi kwenye nguo na pia kama dawa la tiba.

Leo hii shabu na kampaundi za karibu zinatumiwa katika michakato mengi ya tasnia, kwa mfano wakati wa kutengeneza karatasi kiwandani. Myeyusho wa shabu unatumiwa kupunguza hatari za moto ya vitambaa, ubao au karatasi.

Dawa la tiba[hariri | hariri chanzo]

Matumizi ya Shabu yakazidi kuongezeka inaweza ikatumika kama dawa ya kutibu vipele vya ndevu; hili limekuwa tatizo kubwa, hasa kwa wanaume wengi kupata vipele wakati wa kunyoa. Vipele hivyo huwatokea pindi wamalizapo kunyoa na kwa wengine huwa vikubwa kama majipu na pia hukifanya kidevu kuwa cheusi mpaka kwenye mashavu, pia hufanya eneo lililoathirika kuwa gumu sana.

Kwa matatizo yote hayo shabu inao uwezo wa kuondoa vipele sugu vilivyopo eneo la kidevu au vinavyotokea baada ya kunyoa, hivyo shabu inao uwezo wa kutumika pia kama "after shave", pale mhusika anapomaliza kunyoa anaweza kupaka shabu ikamsaidia kuondoa kabisa uwezekano wa vipele kuota na kuondoa ambavyo vilikuwa vimeshaota kidevuni na maeneo ya mashavu.

Tena ina uwezo wa kuondoa fangasi katika sehemu zote za mwili kama miguu, mikono, kichwani, sehemu za siri pamoja na maeneo yote ya mwili wa binadamu na kuurudisha mwili katika hali nzuri zaidi.

Pia shabu ina uwezo wa kutoa chunusi usoni na sehemu nyingine za mwili wa binadamu. Shabu inapochanganyika na vitu vingine kama asali au limao huweza pia kutibu baadhi ya magonjwa ya kina mama ambayo huyapata baada ya kutumia vitu au vipodozi vyenye kemikali nyingi.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shabu kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.