Majadiliano:Johann Sebastian Bach

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

wikipedia imeingiza ubaguzi makala ya muziki wamingizwa wanamuziki wakizungu tu ya waafrika yamefutwa (imeandikwa na mtumiaji:196.45.46.252 17:25, 26 Januari 2009)

Sidhani ya kwamba ni sahihi unachoandika. Angalia Jamii:Wanamuziki wa Tanzania (watu 42) na Jamii:Muziki ya Tanzania (tena wengi). Makala ipi imefutwa?? JB Bach ni kati ya wanamuziki muhimu wa kimataifa na kihistoria hivyo amewekwa katika orodha ya makala za msingi kwa kila wikipedia. Ukitaka kuelewa kwa mfano jina la kundi la "Bush Bach" wa Nairobi (bado haina makala) afadhali ujue Bach ni nani. Halafu ni vema kujiandikisha na kuacha sahihi (niliweka anwani yako hapo juu). --Kipala (majadiliano) 18:30, 26 Januari 2009 (UTC)
Kipala, pole kwa kutomwelewa! Mimi nimemwelewa hivi: Yaani anafikiri humu wanaoandika ni watu maalum tu, na si wengineo. Hivyo uandika mambo ya Wazungu tu kwa kuwa wachangiaji ni Wazungu! Kumbe, wachangiaji wenyewe ndiyo wanahiari ya kuandika makala zile wazipendazo. Kwa makala anazosema za muziki, hasa ni mimi niliyekaa na kusimama kwa pamoja kwenye makala hizo za muziki, ingawa kuna baadhi yao hufanya, lakini si kama vile ninavyofanya. Kingine, wanamuziki Waafrika, wengi hawajulikani. Na hata hao wanaojulikana, nao si type yangu - kuwaandika naona wananizingua kwa sababu sipendi muziki wa bolingo, soukous, zouk, kifupi muziki wa dansi kwa ujumla. Hivyo tumsamehe mwandishi huyo kwani hajui alitendalo! Face-smile-big.svg--Mwanaharakati (Longa) 06:18, 27 Januari 2009 (UTC)
Hakuna cha kusamehe maana hoja si kosa. Ila tu mimi naelewa ya kwamba anamkuta Bach anaona "Ee mbona mzungu hapa" halafu anaandika bila kuchungulia kuna nini tena. Nimetafakarai kama labda tumewahi kufuta makala ambayo haikulingana lakini sikumbuki kitu. Huyu mwandishio akirudi atasoma kama ana akili ataelewa.--Kipala (majadiliano) 08:28, 27 Januari 2009 (UTC)