Nenda kwa yaliyomo

The Magnificent Seven

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Magnificent Seven)
Magnificent Seven
Imeongozwa na John Sturges
Imetayarishwa na John Sturges
Imetungwa na lliam Roberts
Nyota Yul Brynner
Eli Wallach
Steve McQueen
Charles Bronson
Robert Vaughn
James Coburn
Horst Buchholz
Brad Dexter
Muziki na Elmer Bernstein
Imetolewa tar. 23 Oktoba 1960
Ina muda wa dk. 128
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza

The Magnificent Seven ni filamu ya mwaka 1960. Ni moja kati ya filamu za western iliyoongozwa na mwongozaji wa filamu bwana John Sturges. Filamu inazungumzia kundi la watu wanaoenda kukodi wataalamu wa kupambana kwa kutumia silaha kwa lengo la kuwalinda wana kijiji wa Kimexiko dhidi ya maharamia.

Filamu ilitokana na filamu ya awali ya Kijapan chini ya uongozi wake Akira Kurosawa, aliongoza filamu hiyo mnamo mwaka wa 1954, na ilikwenda kwa jina la Seven Samurai. Baadae watu wa Marekani wakafuata mwongozo ule ule wa Kijapani na kubadlisha baadhi ya vielezo vya Kijapani na kuweka vielezo vya Kiwestern ya Amerika.

Muhtasari wa filamu

[hariri | hariri chanzo]

Wanakijiji wa Kimexiko wanajikuta wakivamiwa na majambazi wa kiharamia wanaoongozwa na Calvera (Eli Wallach). Yeye na watu wake wanaingia kijijini na kuleta fujo kubwa, kisha Calvera anaondoka huku akiapa kwamba atarudi siku yoyote bila taarifa.

Kwa hofu ya kurejea kwao, wakuu wa kijiji wanaelekea mpakani mwa mji kununua silaha ili waweze kujilinda. Hata hivyo, wanagundua kuwa wanahitaji msaada wa mtu mwenye uzoefu wa mapigano. Wanamkuta Chris Adams (Yul Brynner), mtaalamu wa silaha, na kumuomba awaongoze.

Chris anawaambia kuwa silaha pekee hazitoshi, kwa sababu wao ni wakulima na si wapiganaji. Ingawa wanamsihi awasaidie, anawajibu kuwa mtu mmoja hawezi kutekeleza mpango huo peke yake.

Kutoka kushoto: Brynner, McQueen, Buchholz, Bronson, Vaughn, Dexter na Coburn – Magnificent Seven.

Licha ya maneno yake, wanakijiji wanaendelea kumtumainia. Hatimaye, Chris anakubali na kuanza kutafuta washirika wa kuungana naye. Anakiri kuwa fedha ndizo msingi wa kuanza kazi hiyo.

Mtu wa kwanza anayemwendea ni Chico (Horst Buchholz), kijana kichwa ngumu asiye na uzoefu mkubwa lakini mwenye ari. Awali anakataa ombi hilo. Anayefuata ni Harry Luck (Brad Dexter), rafiki wa zamani wa Chris, anayekubali kwa kuwa anaamini Chris huwa haendi kwenye kazi bila sababu nzuri ya kifedha. Wa tatu ni Vin (Steve McQueen), anayekubali kwa sababu shughuli zake za kamari zimemfikia ukingoni.

Wengine wanaojiunga ni Bernardo O'Reilly (Charles Bronson), Britt (James Coburn), na Lee (Robert Vaughn), ambaye anatafuta mahali pa kujificha akisubiri hali itulie. Baadaye, Chico pia anarudi na kujiunga na kundi, licha ya awali kukataa.

Washiriki

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: