Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Magnificent Seven

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Glorious Seven

[hariri chanzo]

Muddy makala ni nzuri lakini naona matata kadhaa upande wa kueleweka sawasawa. Lakini hapa mimi niko mbali sina uhakika kama ni tatizo langu tu. Labda umpatie mtu huko uone anachosema. Tatizo ni kama tunatafsiri tunapokea amri za lugha nyingine. Sasa ni swali tufanye nini kama lugha yetu haina dhana mbalimbali kwa mfano "gunslinger", "gunman"? Ni lazima kufuata muundo wa dhana za hadithi ya Kiingereza au heri tuweke haya kando na kusimulia upya? Nimeanza kuandika masahihisho kadhaa lakini inaonekana ingekuwa badiliko kubwa. Kama wenyeji wa huko wanaelewa verma ibaki ilivyo. Menginevyo niambie nitatuma yangu. --Kipala 11:49, 29 Desemba 2007 (UTC)[jibu]


Si vibaya. Lakini hebu fanya tuone kwanza, kisha nitakwambia kama sawa au sisawa. Majadiliano ya hamie hapa--Mwanaharakati 12:15, 29 Desemba 2007 (UTC)[jibu]

Basi hapa maoni kladha sijamaliza.... Angalia kama inaeleweka kirahisi zaidi. Ningefupisha zaidi.

  • "wataalamu wa kupambana na bunduki" - kwangu haieleweki vizuri. Nadhani ni jaribio la kutafsiri "gunmen" - lakini jinsi ilivyo ni zaidi "gun fighting experts" ninchoelewa kama wataalamu katika jitihada za kukandamiza uenezaji wa bunduki haramu nchini. (La sikumaanisha hivyo-Watalaamu wa kupambana kwa kutumia bundiki au Bastola kwa lugha rahisi).
  • "wana kijiji wa Kimexiko" ni sawa lakini ningependelea "wakazi wa kijiji katika Meksiko" kwa sababu kuna Wameksiko hata katika kusini ya Marekani katika maeneo yaliyotwaliwa na Marekani katika vita dhidiy a Meksiko. Hadithi hii yasimuliwa kuhusu kijiji ndani ya Meksiko.
  • "Filamu ilitokana na filamu ya awali ya Kijapan ..." - Labda hivi: Filamu inarudia hadithi ya filamu ya Kijapan ya mwaka 1954 "Seven Samurai" inayosimulia habari za mashujaa wa Samurai katika Japan ya Kale. Hadithi hii yahamishwa katika mazingira ya Amerika ya Kaskazini ya karne ya 19 na badala ya Samurai tunaona macowboy na majambazi Wamerekani. (hapa sawa)


Wakazi wa kijiji cha Mexiko ya Kaskazini wajikuta wakivamiwa matra kwa mara na kundi la majambazi wanaongozwa na Calvera (Eli Wallach). Baada ya kupora kijiji anaahidi ya kwamba atarudi tena. Viongozi wa kijiji wanaamua kununua silaha kwa lengo la kujilinda wenyewe wakisafiri hadi mji wa mpakani na MArekani. Hapa wanakutana na Chris Adams (Yul Brynner) anayedumu maisha yake kama askari wa kukodiwa akiwa hodari sana katika matumizi ya bastola. Adams awaambia kwamba silaha pekee yake hazitaweza kufanya lolote lile la maana kwa sababu wao ni wakulima tu na sio wapiganaji wa kutumia silaha. Wanakiji wamwomba awaongoze katika swala hilo, lakini Chris awakatalia mwanzoni hadi kukubali baadaye. Baada ya kupewa pesa anatafuta wenzake watu wenye uhodari wa kutumia silaha na kukodishwa kwa upiganaji .. .....

Mambo 197.186.27.100 21:36, 29 Julai 2023 (UTC)[jibu]