Papa Gregori XIII : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Minor fix using AWB
d r2.7.1) (Roboti: Imeongeza gd:Pàpa Griogair XIII
Mstari 44: Mstari 44:
[[fi:Gregorius XIII]]
[[fi:Gregorius XIII]]
[[fr:Grégoire XIII]]
[[fr:Grégoire XIII]]
[[gd:Pàpa Griogair XIII]]
[[gl:Gregorio XIII, papa]]
[[gl:Gregorio XIII, papa]]
[[he:גרגוריוס השלושה עשר]]
[[he:גרגוריוס השלושה עשר]]

Pitio la 23:37, 5 Machi 2013

Papa Gregorius XIII

Papa Gregori XIII (*7 Januari 1502 mjini Bologna/Italia; †10 Aprili 1585 mjini Roma) alikuwa papa wa kanisa katoliki kuanzia 13 Mei 1572 hadi kifo chake. Alimfuata Papa Pius V akafuatwa na Papa Sixtus V

Anakumbukwa hasa kwa matengenezo ya kalenda iliyojulikana kama "kalenda ya Gregori" ikawa kalenda ya kimataifa kote duniani.

Alizaliwa kwa jina la Ugo Buoncampagni akafuata masomo ya sheria na kuwa profesa wa sheria kwenye chuo kikuu cha Bologna.

Mwaka 1539 aliitwa na Papa Paulo III akapewa kazi mbalimbali kama mwanasheria wa kanisa. Baadaye Papa Paulo IV alimpa cheo cha askofu wa Viesti (Italia) na ni sasa tu ya kwamba Ugo alikula kiapo cha upadre na kuwekwa wakfu kama askofu moja kwa moja.

Baada ya kifo cha Papa Pius V alichaguliwa kuwa mfuasi wake akachukua jina la "Gregorius". Papa Gregori XIII alijitahidi kurudisha nyuma mwendo wa matengenezo ya kiprotestant. Alikubali kudhulumiwa kwa Wainjili nchini Ufaransa tar. 23 -24 Agosti 1572 ("Usiku wa Bartolomeo"). Alijaribu kukusanya mataifa ya Ulaya dhidi ya Dola la Uturuki kwa shabaha ya kukomboa mji wa Konstantinopoli lakini hakufaulu.

Pamoja na jitihada hizi za kisiasa alijenga taasisi ya taaluma. Aliunda Chuo Kikuu cha Mapapa huko Roma kinachoitwa kwa heshima yake "Gregoriana" hadi leo.

Kalenda mpya hakutunga lakini aliita wataalamu katika kamati maalumu na kukubali mapendekezo yake tar. 24 Februari 1582.

Viungo vya nje

Papa Gregori XIII katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki