Moyo : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d Robot: zh-yue:心 is a featured article
d r2.5) (roboti Nyongeza: am:ልብ
Mstari 61: Mstari 61:


[[af:Hart]]
[[af:Hart]]
[[am:ልብ]]
[[an:Corazón]]
[[an:Corazón]]
[[ang:Heorte]]
[[ang:Heorte]]

Pitio la 18:13, 5 Machi 2012

Moyo wa kibinadamu baada ya kutolewa kwenye maiti kwa utafiti wa kiganga
Moyo kama ishara ya upendo
Muundo wa moyo wa kibinadamu
*1 Vena kava ya juu (damu inaingia kutoka mwilini)
*2 ateri ya mapafu (damu inatoka kwenda mapafu)
*3 vena ya mapafu (damu inarudi kutoka mapafu)
*4 Vali mitralia - 5 Vali ya aorta
*6 Ventrikali kushoto - 7 Ventrikali kulia
*8 Atiria kushoto - 9 Atiria kulia
*10 Aorta (damu inatoka kwenda mwilini)
*11 Vali kwa mapafu - 12 Vali triskupidia
*13 Vena kava ya chini (damu inaingia kutoka mwilini)

Moyo ni ogani ya mwili inayoendesha mzunguko wa damu mwilini. Kazi yake ni kama pampu ya damu. Hali halisi ni musuli inayosukuma damu kwenye mishipa kwa njia ya kujikaza.

Moyo ya mamalia pamoja na binadamu huwa na pande mbili. Upande wa kulia unasukuma damu kwenda mapafu inapopokea oksijeni; upande wa kushoto unazungusha damu katika sehemu nyingine za mwili pale ambako oksijeni inahitajika.

Moyo ni ogani ya lazima kwa uhai.

Moyo na utamaduni

Katika masimulizi ya mataifa wengi moyo inajadiliwa kama mahali pa roho, mawazo au hisia hasa upendo na chuki.

Sababu yake ni ya kwamba pigo la moyo ni dalili la wazi la uhai na bila pigo la moyo mtu amekufa kwa hiyo moyo ilitazamiwa kama mahali pa uhai wenyewe pamoja na nafsi ya mtu.

Siku hizi wataalamu wanaona moyo ni pampu tu ni zaidi ubongo penye mahali pa unafsi wa mtu.

Muhtasari ya kazi ya moyo

(Namba zinalinga na mchoro wa moyo)

Moyo inazungusha damu mwilini.

  • Damu isiyo na oksijeni inafika moyoni (kulia) kutoka viungo. (na. 1+13)
  • Moyo inapeleka damu hii kwenye mapafu inapoongezwa oksijeni. (na. 2)
  • Damu inarudi moyoni (kushoto) ikiwa na oksijeni (na. 3)
  • Kutoka moyoni (kushoto) inasukumwa kwenda mwilini tena na kubeba oksijeni (na. 10)

Muundo wa moyo wa kibinadamu

Moyo wetu huwa na pande mbili na kila upande kuna vyumba viwili. Kwa jumla moyo huwa na vyumba vinne. Amfibia huwa na vyumba vitatu na samaki na vyumba viwili tu.

Damu kutoka mwilini isiyo na oksijeni tena inafika kwenye atiria ya kulia. Atiria inasogeza damu kwenda chumba cha pili au ventrikali ya kulia. Ventrikali inasukuma damu kwenda mapafu inapoongezwa oksijeni. Kutoka mapafu damu yenye oksijeni inarudi moyoni ikiingia atiria ya kushoto na kuendelea ventrikali ya kushoto. Ventrikali hii inasukuma damu mwilini.

Kila sehemu ya kuingia au kutoka kwa damu katika chumba kimoja kuwa na mlango wake na milango hii huitwa "vali" ya moyo. Vali huongezeka jina kufuatana na upande wao ama kulia na kushoto au ya mapafu na menginevyo.

Mishipa ya damu moyoni

Mishipa ya damu moyoni huwa na majina maalumu. Kwa jumla kuna mishipa mikubwa kwa sababu damu yote inapaswa kupita humo. Kwa hiyo mishipa karibu na moyo ni kama barabara kuu za damu mwilini.

Mishipa yote inayopeleka damu kwenda moyoni huitwa "vena". Mishipa yote inayotoa damu kutoka kwa moyo kwenda penginepo huitwa "arteri".

Ateri kuu inayopeleka damu mwilini ni aorta.

Kuna pia ateri za nje zinazozunguka moyo mwenyewe; kama musuli inahitaji oksijeni kwa kazi yake. Ateri za nje zinafikisha damu yenye oksijeni moja kwa moja kwa seli za moyo yenyewe.

Mapigo ya moyo

Pigo la moyo ni hatua ya kujikaza kwa musili ya moyo. Musuli ikijikaza inapunguza nafasi ndani yake na hivyo kusukuma damu kwenda ama chumba kingine kutoka atiri au kwenda mishipa ya damu yaani ateri.

Baadaye musuli inalegea mahali ilipojikaza. Vali inafunguka na damu kutoka vena inaweza kuingia na kujaza chumba cha moyo. Shindikizo ya damu kutoka vena inapanusha chumba tena mpaka kujaa. Sasa vali ya kuingia inafungwa, chumba kinajikaza tena na vali ya kutoka infunguliwa.

Mwendo huu wa kujikaza unasikika kama "pigo la moyo".

Tazama pia

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA