Mtihani : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 6: Mstari 6:

- '''Kabla ya kujiunga na shule au taasisi:''' Hiki ni kipindi ambacho mtahiniwa hupimwa kwa kutolewa mtihani ili kutambuliwa uwezo wake wa kujiunga na shule au taasisi hiyo. Mara nyingi kila shule ina utaratibu wa kumchukua mwanafunzi kutokana na kiwango cha uelewa kwa kutumia alama za maswali zilizowekwa na shule au taasisi hiyo. Ikiwa mtahiniwa atafanikiwa kupata alama zilizowekwa na shule au taasisi husika mtahiniwa huyo ataruhusiwa kujiunga na shule au taasisi hiyo. Mitihani ya namna hii wengi huiita usaili.

- '''Katikati ya masomo au mafunzo:''' Mara nyingi katikati ya masomo au mafunzo husika mwanafunzi hutahiniwa ili kupima uwezo wake wa kile au yale anayojifunza. Mitihani ya namna hii huweza kutolewa kwa ratiba za shule au taasisi husika au mwalimu wa somo anaweza kutoa mitihani ili kupima uwezo wa wanafunzi wake. Mitihani ya namna hii ni muhimu sana, kwani humsaidia mwalimu kuelewa uwezo wa mwanafunzi wake na hata mwanafunzi mwenyewe kujitathmini kiwango cha uelewa wake.

- '''Mwisho wa masomo/mafunzo:''' Mara baada ya kumaliza masomo au mafunzo mwanafunzi hupewa mtihani ili kumpima juu ya yale yote aliyojifunza. Kwa baadhi ya nchi au nchi nyingi duniani hutumia mitihani ya mwisho kama ni upimaji utakaomwezesha mwanafunzi kupata cheti cha kuhitimu mafunzo yake. Maranyingi, kushindwa kwa mtihaani wa mwisho ni kushindwa kwa masomo yake. Mitihani ya namna hii hutolewa na taasisi maalumu kama vile Baraza la mitihani la Taifa kwa nchi ya Tanzania na taasisi nyingine zenye dhamana ya kufanya hivyo.

Pitio la 21:15, 11 Desemba 2019

Mtihani ni njia ambayo mtu anapimwa kutokana na alichokisoma au alichofundishwa ili atambuliwe kwamba alielewa au hakuelewa. Au ni kipimo cha maisha kutokana na ulichojifunza.

Katika shule mwanafunzi hupimwa na walimu wake juu ya kile walichomfundisha ili kumjua kama anaelewa au haelewi.

Mitihani yaweza kuwa migumu au rahisi kutokana na mwanafunzi mwenyewe: kama huwa hajisomei ataiona migumu na kama anajisomea ataiona rahisi hata kama mwalimu alitunga migumu kiasi gani.Kama tujuavyo, lengo la mtihani kwa mwanafunzi ni kumpima kile alichojifunza kutoka chanzo cha mafunzo yake, baada ya kipimo hicho ndipo mwanafunzi anaweza kufanyiwa tathmini ya kumjua kama anafaa kwa lipi na hafai kwa lipi. Kitaaluma, hasa katika masuala ya shule, mwanafunzi anaweza kupimwa katika vipindi vikuu vitatu:

- Kabla ya kujiunga na shule au taasisi: Hiki ni kipindi ambacho mtahiniwa hupimwa kwa kutolewa mtihani ili kutambuliwa uwezo wake wa kujiunga na shule au taasisi hiyo. Mara nyingi kila shule ina utaratibu wa kumchukua mwanafunzi kutokana na kiwango cha uelewa kwa kutumia alama za maswali zilizowekwa na shule au taasisi hiyo. Ikiwa mtahiniwa atafanikiwa kupata alama zilizowekwa na shule au taasisi husika mtahiniwa huyo ataruhusiwa kujiunga na shule au taasisi hiyo. Mitihani ya namna hii wengi huiita usaili.

- Katikati ya masomo au mafunzo: Mara nyingi katikati ya masomo au mafunzo husika mwanafunzi hutahiniwa ili kupima uwezo wake wa kile au yale anayojifunza. Mitihani ya namna hii huweza kutolewa kwa ratiba za shule au taasisi husika au mwalimu wa somo anaweza kutoa mitihani ili kupima uwezo wa wanafunzi wake. Mitihani ya namna hii ni muhimu sana, kwani humsaidia mwalimu kuelewa uwezo wa mwanafunzi wake na hata mwanafunzi mwenyewe kujitathmini kiwango cha uelewa wake.

- Mwisho wa masomo/mafunzo: Mara baada ya kumaliza masomo au mafunzo mwanafunzi hupewa mtihani ili kumpima juu ya yale yote aliyojifunza. Kwa baadhi ya nchi au nchi nyingi duniani hutumia mitihani ya mwisho kama ni upimaji utakaomwezesha mwanafunzi kupata cheti cha kuhitimu mafunzo yake. Maranyingi, kushindwa kwa mtihaani wa mwisho ni kushindwa kwa masomo yake. Mitihani ya namna hii hutolewa na taasisi maalumu kama vile Baraza la mitihani la Taifa kwa nchi ya Tanzania na taasisi nyingine zenye dhamana ya kufanya hivyo.

Sifa za mwanafunzi

  • 1) Mwanafunzi kama hajaelewa anatakiwa kuuòiza bila ya kuogopa kupigwa
  • 2) Anatakiwa kuwaheshimu walimuj na wanafunzi wenzake ili ajenge upendo baina yao
  • 3) Ajenge ushirikiano na wenzake katika kufanya kazi walizopewa
  • 4) Kama amepewa mtihani asimsaidie/asisaidiwe maana ni kipimo cha uelewa wao
  • 5) Mwanafunzi anatakiwa afanye kazi alizopewa kwa muda aliopangiwa bila kuchelewa.

Mwanafunzi akifaulu mtihani tunasema kuwa alielewa na hupewa zawadi na walimu na wazazi nyumbani kama pongezi, hivyo basi mwanafunzi anapopewa zawadi hujijengea kwamba ili apewe zawadi inambidi asome kwa bidii sana.

Katika shule huwa na mashindano ya wanafunzi ili waweze kumpata wa kwanza kati yao. Mitihani hutungwa na walimu wenyewe. Huwa na mtihani wa wiki, mwezi, robo mhula, nusu mhula na mtihani wa mwisho.

Katika mitihani asilimia kubwa ya wanafunzi huwa na woga, ndiyo maana hupewa mitihani shuleni ili waizoee.

Nchini Tanzania kuna mtihani wa taifa: mtihani huo humvusha mwanafunzi katika daraja alilopo na kwenda katika hatua nyingine (kutoka shule ya msingi kwenda sekondari, kutoka sekondari kwenda chuo kikuu na hatimaye kufaulu na kutimiza malengo yako).

Faida za mitihani

  • 1) Kwanza humfanya mtu azoee kitu fulani
  • 2) Humwondolea mwanafunzi uwoga juu ya kitu anachokifanya, n.k.

Ili tufaulu mitihani tunatakiwa tusome sana na kwa bidii juhudi kubwa sana.

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtihani kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.