Nenda kwa yaliyomo

Luis Diaz (mchezaji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mshambuliaji winga Luis Diaz akiwa na timu yake ya LIverpool ya UIngereza

Luis Fernando Díaz Marulanda (alizaliwa 13 Januari 1997) ni mwanasoka wa kulipwa wa Kolombia ambaye anacheza katika nafasi ya winga ama kiungo winga wa klabu ya Liverpool F.C. ya nchini Uingereza, na timu ya taifa ya Kolombia.

Díaz alianza safari yake ya soka katika Divisheni ya Pili ya kolombia huko Barranquilla kabla ya kuhamia Atlético Junior, akishinda Categoria Primera A, Copa Colombia moja na Superliga Colombiana moja. Mnamo 2019, alijiunga na FC Porto kwa ada iliyoripotiwa ya Euro milioni 7, akishinda mara mbili Primeira Liga na Taça de Portugal, na Supertaça Cândido de Oliveira moja. Baada ya mabao 14 ya ligi katika mechi 18 za ligi hio, klabu ya Liverpool ilimsajili katika kipindi cha kwanza cha 2021-22, kwa uhamisho wa thamani ya €45 milioni (£37.5 milioni)[1][2]. Alishinda Kombe la EFL na Kombe la FA katika msimu wake wa kwanza, na alikuwa mchezaji bora wa mechi katika Fainali ya Kombe la FA 2022.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Carroll, James (30 Januari 2022). "Liverpool complete Luis Diaz transfer from FC Porto". Liverpool F.C. Iliwekwa mnamo 30 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Diaz joins Liverpool from Porto for £37.5m", BBC Sport. 
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Luis Diaz (mchezaji) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.