Nenda kwa yaliyomo

Luis Amigo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Luis Amigò)
Askofu Luis Amigó

Luis Amigó y Ferrer alikuwa askofu wa jimbo katoliki la Segorbe na mtawa wa Ndugu Wadogo Wakapuchini.

Alizaliwa Masamagrell (Valencia huko Hispania) tarehe 17 Oktoba 1854 akafa Godella (Valencia) tarehe 1 Oktoba 1934.

Biografía

[hariri | hariri chanzo]

Alijiunga na shirika la Wakapuchini mwaka 1874 huko Bayonne (Ufaransa).

Aliporudi Hispania, mwaka 1879, Luis Amigó alipewa daraja takatifu ya upadri.

Tarehe 11 Mei 1885 alianzisha shirika la Masista Watersiari Wakapuchini wa Familia Takatifu na miaka minne baadaye, tarehe 12 Aprili 1889, shirika la kiume la Watersiari Wakapuchini wa Bikira Maria wa Mateso.

Tarehe 9 Juni 1907, aliwekwa wakfu kuwa askofu wa jimbo la Solsona, hata 1913, alipopewa jimbo la Segorbe, alipobaki hadi 1934, alipofariki.

Kesi ya kumtangaza mwenye heri imefikia hatua ya kutangazwa kwamba alitimiza maadili yote kwa ushujaa.