Lucy Liu
Lucy Liu | |
---|---|
| |
Jina la kuzaliwa | Lucy Alexis Liu |
Alizaliwa | 2 Desemba 1968 |
Kazi yake | Mwigizaji |
Miaka ya kazi | 1991 – Hadi leo |
Lucy Alexis Liu (amezaliwa 2 Desemba 1968) ni mshindi wa Tuzo ya Emmy kama mwigizaji bora filamu wa Marekani. Lucy alianza kujipataia umaarufu ni baada ya kucheza katika mfululizo wa kipindi cha televisheni cha Ally McBeal (1998–2002) na pia kuonekana katika baadhi ya filamu maarufu kama vile Chicago, Kill Bill na Charlie's Angels.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa na kukua akiwa na kaka yake, Alex Liu, mjini Jackson Heights, Queens, New York na wahamiaji wa Kichina.[1] Liu alisema kwamba yeye alilelewa na kukulia katika maisha ya maliwazo ya majirani.[1] Familia yake inazungumza Kimandarin. Lucy Liu hakujifunza Kiingereza hadi alipofikisha umri wa miaka mitano.[2] Baba yake, Tom, alikuwa mhandisi wa kujitegemea na mama yake, Cecilia, ni mwanabiokemia mjini Taiwan, lakini walizotoa sadaka kazi hizo na badala yake wakaelekea nchini Marekani.
Baada ya wazazi wa wake kutalikana, Liu ikamlazimu kutafuta muda wa kuweza kujipatia elimu. Alisoma katika shule ya Joseph Pulitzer Middle School (I.S.145) na kuja kumaliza katika shule ya mjini New York Stuyvesant High School kunako mwaka wa 1986.[3] Baada ya hapo akaelekea zake kujiunga na masomo ya chuo kikuu cha New York kwa mwaka mmoja, kabla ya kuhamishwa katika chuo kikuu cha Michigan ambapo alimaliza elimu yake na kupata digrii ya sayansi na lugha za Kiasia na tamaduni zake.
Televisheni
[hariri | hariri chanzo]- Beverly Hills, 90210 - Msimu 2, Sehemu ya 6 - "Pass, Not Pass" (1991)
- L.A. Law - Msimu 8, Sehemu ya 4 - "Foreign Co-respondent" (1993)
- Hotel Malibu - Msimu 1, Sehemu ya 2 - "Do Not Disturb" (1994)
- Coach - Msimu 7, Sehemu ya 2 - "It Should Happen to You" (1994)
- Coach - Msimu 7, Sehemu ya 11 - "Out of Control" (1994)
- Home Improvement - Msimu 4, Sehemu ya 16 - "Bachelor of the Year" (1995)
- Hercules: The Legendary Journeys - Msimu 1, Sehemu ya 8 - "The March to Freedom" (1995)
- ER - Msimu 2, Sehemu ya 3 - "Do One, Teach One, Kill One" (1995)
- ER - Msimu 2, Sehemu ya 4 - "What Life?" (1995)
- ER - Msimu 2, Sehemu ya 5 - "And Baby Makes Two" (1995)
- Nash Bridges - Msimu 1, Sehemu ya 1 - "Genesis" (1996)
- The X-Files - Msimu 3, Sehemu ya 19 - "Hell Money" (1996)
- High Incident - Msimu 1, Sehemu ya 6 - "Father Knows Best" (1996)
- High Incident - Msimu 1, Sehemu ya 7 - "Follow the Leader" (1996)
- NYPD Blue - Msimu 4, Sehemu ya 17 - "A Wrenching Experience" (1997)
- Ally McBeal - Msimu 2-5 (regular) (1998–2002)
- Sex and the City - Msimu 4, Sehemu ya 11 - "Coulda, Woulda, Shoulda" (2001)
- Joey - Msimu 1, Several Sehemu yas (2004-2005)
- Ugly Betty - Msimu 1, Sehemu ya 16 - "Derailed" (2007)
- Ugly Betty - Msimu 1, Sehemu ya 17 - "Icing on the Cake" (2007)
- Traffic: An MTV EXIT Special - Host of an MTV documentary to raise awareness about human trafficking in Asia (2007)
- "Cashmere Mafia"
- "The Simpsons"
- Futurama Msimu 3, Sehemu ya 15, Starring as herself (and robot copies of herself)[4]
Filamu
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 Roberts, Sheila (2006-12-21). "Lucy Liu Interview, CodeName The Cleaner". Movies Online. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-01-06. Iliwekwa mnamo 2006-12-21.
{{cite news}}
: Check date values in:|date=
(help); Cite has empty unknown parameter:|coauthors=
(help) - ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-01-10. Iliwekwa mnamo 2008-07-17.
- ↑ Ogunnaike, Lola (2003-10-13). "The Perks and Pitfalls Of a Ruthless-Killer Role; Lucy Liu Boosts the Body Count in New Filamu". New York Times. Iliwekwa mnamo 2007-11-01.
{{cite news}}
: Check date values in:|date=
(help) - ↑ "Futurama" I Dated a Robot (2001)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Lucy Liu kwenye Internet Movie Database
- Lucy Liu katika TV.com