Nenda kwa yaliyomo

Tembe ya Livingstone

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Livingstone's Tembe)

Tembe ya Livingstone au Makumbusho ya David Livingstone, Tabora (Livingstone's Tembe kwa Kiingereza) ni eneo la kihistoria la kitaifa lililopo karibu na kijiji cha Kwihara kilichoko katika Wilaya ya Tabora Mjini, mkoani Tabora.

Nyumba hiyo ilijengwa mwaka 1857. David Livingstone aliishi hapo kwa sehemu ya mwaka 1871. Baadaye mwaka huo [Upelelezi|Mpelelezi]] Henry Morton Stanley alikaa hapo kwa miezi mitatu kwa matumaini kuwa Waarabu wangeangamiza Mtemi Mirambo, kiongozi mashuhuri wa kabila la Wanyamwezi (Watu wa Mwezi), na kufungua njia ya kwenda Ziwa Tanganyika. Baada ya Mirambo kushinda, Stanley alilazimika kutumia njia ya Mpanda kwenda Ujiji. Mwaka uliofuata, Stanley na Livingstone walirudi pamoja katika tembe hiyo.

Kwa sasa, ni makumbusho na ina milango ya Kiswahili iliyochongwa kwa ustadi, barua kadhaa zilizotumwa na David Livingstone, na maelezo kuhusu biashara ya utumwa.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]