Lilian Mary Nabulime

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
lilian Mary Nabulime
Amezaliwa 22
Uganda
Nchi Uganda
Kazi yake Ni mhariri wa Sanaa na mchongaji wa sanamu
Lilian Mary Nabulime
Lilian Mary Nabulime

Lilian Mary Nabulime (alizaliwa 22 Desemba 1963) ni mhadhiri wa sanaa na mchongaji wa sanamu nchini Uganda. Ni mhandisi wa chuo cha uundaji, sanaa na teknolojia (CEDAT) na amefanya maonyesho ya kazi zake ndani na nje ya nchi yake. [1]

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Nabulime alizaliwa wilaya ya Kampala nchini Uganda mwaka 1963 na kusoma shule ya msingi ya wasichana Nkoni. Alisoma shule ya Makerere kwa elimu ya sekondari na upili na baadae kupata shahada ya Sanaa kutoka Chuo kikuu cha Makerere mwaka 1987. Alipata shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Makerere na shahada ya uzamivu katika chuo kikuu cha Newcastle mwaka 2007.[2]

Kazi yake[hariri | hariri chanzo]

Nabulime ni mhadhiri na pia alishawahi kuwa kiongozi wa idara ya viwanda, Sanaa, chuo cha uhandisi, uundaji, na teknolojia (CEDAT) katika chuo kikuu cha makerere. Kazi yake hutumia vitu vya kawaida kama vile sabuni, chujio, nguo, chupa za chuma na sehemu za magari katika kutengeza taswira na ajenda zinazohusu magonjwa, jinsia na mazingira kwa lengo la kuongeza utambuzi na kuikuza Sanaa.[3][4]

Tuzo zake[hariri | hariri chanzo]

  • Commonwealth Fellowship Award UK (2012)[5]
  • Robert Sterling Fellowship, Vermont Studio Center, USA (2011)
  • African Stones Talk Sculpture Symposium (AST), Kenya (2011);
  • British Academy International Visiting Fellowship 2009;[6]
  • ROLS UK (2009 and 2008) and; Commonwealth Fellowship Award, UK (1997).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Lillian Mary Nabulime". 
  2. "The role of sculptural forms as a communication tool in relation to the lives and experiences of women with HIV/AIDS in Uganda.". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-07. Iliwekwa mnamo 2021-03-06.  Unknown parameter |= ignored (help)
  3. "Lillian Nabulime addresses girl child in exhibition". 
  4. "Nabulime’s bold and beautiful art lights up the work place". Retrieved on 2021-03-06. Archived from the original on 2018-04-29. 
  5. "Using Art to talk about HIV/AIDS". 
  6. "Using art and everyday objects to fight HIV/AIDS in Uganda". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-01-28. Iliwekwa mnamo 2021-03-06.  Unknown parameter |= ignored (help)