Leandro Paredes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Leandro Peredes akiwa AS Roma

Leandro Daniel Paredes (alizaliwa 29 Juni 1994) ni mchezaji wa soka wa Argentina ambaye anacheza kama kiungo wa kati wa klabu ya Ufaransa Paris Saint-Germain FC.

Paredes alianza kazi yake katika chuo cha mafunzo cha Boca Juniors akiwa na umri wa miaka 14. Aliendelea kuwa katika kiwango chake na baadae kuchukuliwa kwa mkopo na klabu ya Italia AS Roma, Mnamo tarehe 19 Julai 2014 Paredes alijiunga na Roma kwa mkataba wa muda mfupi kwa Milioni 6.5.

Mnamo tarehe 1 Julai 2017, Zenit saint Petersburg ilitangaza kusainiwa mkataba wa miaka minne na Peredes kwa ada ya € milioni 27. Mnamo tarehe 29 Januari 2019, klabu ya Ufaransa Paris Saint-Germain ilitangaza kusainiwa mkataba wa miaka minne na nusu na Peredes kwa € Milioni 47.

Mei 2018 aliitwa jina kwenye kikosi cha Argentina cha kwanza ili kucheza Kombe la Dunia la 2018 nchini Urusi.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Leandro Paredes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.