Lashinda Demus
Lashinda Demus (alizaliwa 10 Machi 1983 mjini Inglewood, California) ni mwanariadha wa urukaji viunzi ambaye ni mtaalamu wa mbio ya 400m ya kuruka viunzi.
Muda wake bora wa kibinafsi katika mbio ya 400m ni 53.02s,aliohitimu katika mwezi wa Julai 2006 jijini Athens.
Yeye alikuwa katika Long Beach Wilson alipokimbia na bado anashikilia rekodi ya mbio ya 300m ya kuruka viunzi. Alikimbia pia mbio ya 4 x 400, 4 x 100 na ,vilevile, mbio fupifupi.
Baada ya shule ya sekondari, Lashinda alihudhuria Chuo Kikuu cha Carolina Kusini kukimbia chini ya kocha Curtis Frye. Muda wake bora akiwa chuo kikuu:
- mbio ya 55m ya urukaji viunzi: 7.80
- mbio ya 60m ya urukaji viunzi: 8.32
- mbio ya 100m ya urukaji viunzi: 13.35
- mbio ya 400m ya urukaji viunzi : 54.70
- mbio ya 400m: 51.38
- mbio ya 800m: 2:13.77
Akitupilia mbali kumbukumbu za kushindwa hapo awali katika kuhitimu Olimpiki ya 2008 , alishinda Mashindano ya Mabingwa wa Marekani ya 2009 katika mbio ya 400m ya urukaji viunzi.Alishinda na muda wa sekunde 53.78 na kushinda nafasi ya kucheza katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2009. Aliboresha muda wake katika mbio za mashindano ya Herculis katika mwezi wa Julai ukawa sekunde 52.63. Hii ilikuwa rekodi katika mashindano hayo na muda wa kasi wa nne katika tukio hilo.
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Mashindano | Pahali pa kushindana | Matokeo | Maelezo ya ziada |
---|---|---|---|---|
2002 | Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Vijana ya 2002 | Kingston, Jamaica | 1 | |
2005 | Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2005 | Helsinki, Finland | 2 | |
Mashindano ya Riadha ya IAAF | Monte Carlo, Monaco | 1 | ||
2006 | Mashindano ya Riadha ya IAAF ya 2006 | Stuttgart, Ujerumani | 1 | |
Mashindano ya Riadha ya IAAF ya Kombe la Dunia ya 2006 | Athens, Ugiriki | 2 |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- http://gamecocksonline.cstv.com/sports/c-track/mtt/demus_lashinda00.html Ilihifadhiwa 6 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine..
- Morse, Parker (2009-06-28). World season leads for Demus and Merritt as team takes shape in Eugene - USA Champs, Siku ya tatu. IAAF.
- Turner, Chris (2009-07-28). Hurdlers delight on a spectacular evening in Monaco - IAAF World Athletics Tour. IAAF.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- IAAF wasifu wa Lashinda Demus