Lango:Hip hop/Wasifu uliochaguliwa/Snoop Doggy
Cordozar Calvin Broadus, Jr (amezaliwa, 20 Oktoba 1971) ni Rapa wa kimarekani na pia muigazaji wa filamu. Alipata umaarufu kama Snoop Dogg, mwanzoni walikuwa wakimuita Snoop Dogg Doggy.
Akiwa anawakilisha kikosi cha West Coast Hip Hop, pamoja na mshirika wake wa karibu bwana Dr. Dre ambaye ndiye aliyesababisha Snoop kuwa hapo alipofikia. Snoop kuna misemo yake ambayo imezoleka sana midomoni mwa watu vile akisema 'fo' Shizzle, manizzle, akimanisha, kweli ndugu yangu, useme huo ulibuniwa na mwanamuziki mmoja wa huko huko nchini marekani maarufu kama Frank Smith & the Band, mnamo miaka ya 80 hivi.
Snoop alizaliwa mjini Long Beach, California tar. 20 Oktoba 1971.
Akiwa bwana mdogo alipata jina la Snoop ambalo alipewa na mama yake mzazi kama jina la utani kwakuwa alikuwa anapenda kutazama kipindi cha televisheni kilichokuwa kinaitwa "Peanuts", kipindi ambacho kiliegemea kwenye masuala ya "Ucheshi", likiwemo na jina fulani la Snoop Dogg.
Snoop ajiunga na shule ya Long Beach Polytechnic High School, na baadae akapelekwa