Lango:Hip hop/Wasifu uliochaguliwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Tupac akiwa Studio

'Tupac Amaru Shakur (16 Juni 1971 - 13 Septemba, 1996) alikuwa mwigizaji, mwanaharakati wa haki za binadamu, na pia mwanamuziki maarufu wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama 2Pac. Ni mmoja kati ya wasanii wa hip hop waliouza rekodi nyingi za muziki dunia.

Huyu alikuwa mtoto wa Afeni Shakur, ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha Black Panther Party. Mama yake Tupac alitolewa jela mwezi mmoja kabla ya kumzaa Tupac. Tupac alikufa mnamo tar. 13 Septemba katika mwaka wa 1996 baada ya kupigwa risasi akiwa anaendesha gari mjini Las Vegas, Nevada, siku saba kabla kifo chake.

Mara nyingi aliitwa 2Pac, Pac, Makaveli na pia mwenyewe akajiita The Don Kiluminati. Tupac, pia alishawahi kuishikiria Guinness World Record kwa kuwa na mauzo ya juu sana kwa msanii wa muziki wa rap/hip hop. Alipata mauzo takriban milioni 74 kwa hesabu ya dunia nzima na milioni 44 kwa mauzo ya Marekani pekee.

Soma zaidi....