Mtolondo
Mandhari
(Elekezwa kutoka Lagonosticta)
Mtolondo | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Dume la Mtolondo domo-jekundu
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 11:
|
Mitolondo au bwerenda ni ndege wadogo wa jenasi Lagonosticta katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika tu. Wanafana na mishigi lakini madume wana rangi za nyekundu, kahawa na kijivu, pengine pamoja na madoa meupe madogo. Majike wana rangi za kahawa na kijivu kwa kawaida lakini mara nyingi wana sehemu nyekundu pia na madoa meupe kidarini. Hula mbegu hasa na wadudu pia, hususa makinda. Tago lao ni tufe la manyasi na majani lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 3-6. Spishi nyingi ni wateswa wa vinili ambao huyataga mayai yao katika matago ya mitolondo.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Lagonosticta landanae, Mtolondo wa Landana (Landana Firefinch)
- Lagonosticta larvata, Mtolondo Uso-mweusi (Black-faced Firefinch)
- Lagonosticta nitidula, Mtolondo Kahawia (Brown Firefinch)
- Lagonosticta rara, Mtolondo Tumbo-jeusi (Black-bellied Firefinch)
- Lagonosticta rhodopareia, Mtolondo wa Jameson (Jameson's Firefinch)
- Lagonosticta rubricata, Mtolondo biliwili (African Firefinch)
- Lagonosticta rufopicta, Mtolondo Kidari-madoa (Bar-breasted Firefinch)
- Lagonosticta sanguinodorsalis, Mtolondo-miamba (Rock Firefinch)
- Lagonosticta senegala, Mtolondo Domo-jekundu (Red-billed Firefinch)
- Lagonosticta umbrinodorsalis, Mtolondo wa Chadi (Chad Firefinch)
- Lagonosticta virata, Mtolondo wa Mali (Mali Firefinch)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Dume la mtolondo uso-mweusi
-
Dume la mtolondo kahawia
-
Dume la mtolondo tumbo-jeusi
-
Dume la mtolondo wa Jameson
-
Jike la mtolondo wa Jameson
-
Dume la mtolondo biliwili
-
Jike la mtolondo biliwili
-
Jike la mtolondo kidari-madoa
-
Dume la mtolondo-miamba
-
Jike la mtolondo domo-jekundu
-
Jike la mtolondo wa Chadi