Nenda kwa yaliyomo

Kuhariri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuhariri ni mchakato wa kuchagua na kuandaa nyenzo za maandishi, picha, sauti na filamu zinazotumiwa na mtu au chombo kuwasilisha ujumbe na taarifa. Mchakato wa kuhariri husisha kusahihisha, kuunganisha, kupunguza na kufanya marekebisho mengine kwa lengo la kutoa kazi sahihi na thabiti.

Kuhariri huanza na wazo la mwandishi kwa ajili ya kazi yenyewe, na huendelea pale ambapo huyo humshirikisha mhariri, na kazi huanza.[1][2]

Kuna vyeo tofauti tofauti za wahariri kwenye uchapishaji. Kwa kawaida utakuta wahariri wasaidizi hutoa ripoti kwa wahariri nguli na wakurugenzi ambao huripoti kwa wahariri watendaji. Wahariri watendaji wana jukumu la kuendeleza kazi hadi toleo lake la mwisho. Kwa kadiri chapisho linavyokuwa dogo ndivyo majukumu ya kuhariri huingiliana.

  1. "editing definition - Dictionary - MSN Encarta". web.archive.org. 2009-10-22. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-22. Iliwekwa mnamo 2022-09-29.
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-06. Iliwekwa mnamo 2022-09-29.