Kristen Hager
Kristen Hager | |
---|---|
Amezaliwa | 4 Aprili 1984 Red Lake, Ontario, Kanada |
Kazi yake | Mwigizaji |
Miaka ya kazi | 2005 – hadi leo |
Kristen Hager (amezaliwa tar. 4 Aprili 1984)[1] ni mwigizaji wa filamu na tamthiliya kutoka nchini Kanada.
Wafisu
[hariri | hariri chanzo]Maisha na sanaa
[hariri | hariri chanzo]Hager alizaliwa mjini Red Lake, Ontario na urithi wa Kijerumani.[2] Hager Alianza kuonekana kwa mara kwanza katika mfululizo mdogo wa kipindi cha televisheni cha Beach Girls mnamo 2005. Baada ya mwaka mmoja akaja kuonekana tena katika mfululizo mwingine wa kipindi cha televisheni maarufu kama Runaway, ambamo amecheza nyota Donnie Wahlberg na mwigizaji mtoto Niamh Wilson.
Pia amepata kuonekana katika ugawaji wa Tuzo za Golden Globe kwa ajiri ya filamu ya I'm Not There. Mwonekano wake uliyomkubwa kabisa ni pamoja na kuonekana katika mfululizo wa filamu za Aliens vs. Predator: Requiem, ambayo ya awali ilikuwa Alien vs. Predator.
Hager amecheza kama Cathy katika tamhilia ya mwaka wa 2008 maarufu Wanted. Hager kwa sasa anatengeneza filamu nyingine mbili ambazo zinategemewa kutoka mwishoni mwa mwaka wa 2008, zote mbili wanazitengenezea matangazo yake.
Filamu
[hariri | hariri chanzo]- Of Murder and Memory (2008) (TV) .... Aimee Linden
- You Might as Well Live (2008) .... Cookie
- Wanted (2008) .... Cathy
- Sophie (sehemu ya 1, Guess Who's Coming to Dinner?, 2008) .... Miriam Cambridge
- The Dresden Files (sehemu ya 1, Unaired Pilot: Storm Front, 2008) .... Polly
- Aliens vs. Predator: Requiem (2007) .... Jesse
- St. Urbain's Horseman (2007) TV mini-series .... Ingrid
- I'm Not There (2007) .... Mona/Polly
- Runaway (2 episodes, Pilot and Identity Crisis, 2006) .... Kylie
- Recipe for a Perfect Christmas (2005) (TV) .... Morgan
- Beach Girls (2005) TV mini-series .... Skye
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Kristen Hager MAHALO". Mahalo.com. Iliwekwa mnamo 2008-08-15.
- ↑ "Kristen Hager Joins the Cast of AVP: Survival of the Fittest". MovieWeb. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-24. Iliwekwa mnamo 2006-10-16.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kristen Hager at the Internet Movie Database
- Kristen Hager katika Movies.com