Krioli ya Guyana ya Kifaransa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Krioli ya Guyana ya Kifaransa ni lugha ya Krioli inayotumiwa hasa katika Guyana ya Kifaransa na katika nchi jirani za Surinam na Guyana. Kwa Kifaransa inaitwa Créole guyanais au Guyanais, wenyewe wanasema Kriyòl Gwiyannen.

Ni lugha ya Krioli yenye asili katika Kifaransa, pamoja na athira za lugha za Kiafrika, Kiindio, na Kireno. Inafanana na Krioli ya Visiwa vya Karibi: kuna tofauti za msamiati na sarufi lakini kwa jumla wasemaji huelewana.

Lugha hiyo ni tofauti na Krioli ya nchi jirani Guyana (Guyanese Creole) ambayo ni lugha yenye asili ya Kiingereza.

Mifano[hariri | hariri chanzo]

Mifano[hariri | hariri chanzo]

Kikrioli cha Guyana ya Kifaransa
/matamshi/
Kifaransa sanifu Kiswahili
Bonswè /bõswɛ/ Bonsoir Jioni njema! (habar za jioni)
Souplé /suːple/ S'il vous plaît Tafadhali
Mèsi /mɛsi/ Merci Asante
Mo /mo/ Moi, me, je Mimi
To /to/ Toi, te, tu Wewe
I, L, Li /i, l, li/ Lui, le, la Yeye
Roun /ʁuːn/ Un, une Moja
Eskizé mo /ɛskize mo/ Excusez-moi Unisamehe
Lapli ka tonbé /laˈpliː ka tõbe/ Il pleut mvua inanyesha
Jod-la a roun bèl jou /ʒodˈla a ruːn bel ʒu/ Aujourd'hui, il fait beau Leo ni siku nzuri
A kouman to fika? /a kumã to fika/ (Comment) ça va? habari zako?
Mari a mo manman /maʁi a mo mãˈmã/ Marie est ma mère Maria ni mama yangu
Rodolf a to frè /ʁodolf a to frɛ/ Rodolphe est ton frère Rodolf ni kaka yako
I ka alé laplaj /i kaːle laˈplaʒ/ Il va à la plage Anakwenda mwambaoni
Mo pa mélé /mo pa mele/ Je m'en moque Sijali

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Krioli ya Guyana ya Kifaransa kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.