Nenda kwa yaliyomo

Kontua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya njia za kupanda Kilimanjaro inaonyesha mistari ya kontua.
Ramani hii ya Kilimanjaro huwa na rangi tofauti zinazofuata kontua, bila kuonyesha mistari.

Kontua (kutoka Kiingereza: contour, contour line, pia isoline) ni mstari unaotumiwa kwenye ramani kuunganisha sehemu zilizo na kimo sawa juu ya usawa wa bahari. Kila mstari hupangwa kwa kimo fulani, na tofauti hutegemea skeli ya ramani.

Kwenye ramani ya bahari kontua zinaweza kuonyesha kina chini ya usawa wa bahari.

Kwa hiyo mistari ya kontua zinaonyesha jinsi gani eneo linapanda juu au kutelemka. Kama mistari iko karibu sana mtelemko ni mkali; kama eneo linapanda polepole umbali baina ya mistari ya kimo tofauti ni kubwa zaidi. Pale ambapo mistari ya kontua inakutana mahali pamoja kuna mtelemko mkali wa ghafla.

Mistari ya kontua hutumiwa pia katika ramani za hali ya hewa zinazoonyesha maeneo yenye kanieneo tofauti au maeneo yenyo jotoridi tofauti.

Matumizi ya mistari ya kontua

[hariri | hariri chanzo]

Ramani za kontua huweza kubainisha matumizi mbalimbali ya ardhi kwa watu waishio mahali fulani. Kwa mfano, shughuli za kilimo, ujenzi wa barabara, uchimbaji wa madini, mifereji na utengenezaji wa matuta ili kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Kukaribiana kwa mistari ya kontua

[hariri | hariri chanzo]

Mistari ya kontua huweza kukaribiana lakini haiwezi kugusana wala kuungana. Mistari ya kontua inapokaribiana hudhihirisha mwinuko mkali na inapokuwa mbalimbali huonyesha mwinuko wa kadiri au tambarare.

Ni mistari ya kontua inapokuwa na umbo la V au U kuelekea juu kwenye mwinuko.

ni sehemu ya ardhi iliyo tambarare kati ya vilele au safu za milima. Pitio huonekana katika kontua kati ya vilele au safu za milima. Reli au barabara huweza kupitishwa sehemu hizo. Katika nchi zenye milima watu watembeao kwa miguu hupita humo.

Uwanda wa juu

[hariri | hariri chanzo]

Ni sehemu ya ardhi iliyoinuka na ardhi yake ni tambarare au ina vilima na miinuko ya hapa na pale. Katika nchi ya Tanzania sehemu hizo ni kama vile Dodoma,Tabora, Iringa, Shinyanga.

Ni mistari ya kontua inapokaribiana sana kama vile inakaribia kukutana huonesha kuwa mwinuko wa ardhi katika sehemu hiyo ni mkali


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: