Kontua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani ya njia za kupanda Kilimanjaro inaonyesha mistari ya kontua.
Ramani hii ya Kilimanjaro huwa na rangi tofauti zinazofuata kontua, bila kuonyesha mistari.

Kontua (kutoka Kiingereza: contour, contour line, pia isoline) ni mstari unaotumiwa kwenye ramani kuunganisha sehemu zilizo na kimo sawa juu ya usawa wa bahari. Kila mstari hupangwa kwa kimo fulani, na tofauti hutegemea skeli ya ramani.

Kwenye ramani ya bahari kontua zinaweza kuonyesha kina chini ya usawa wa bahari.

Kwa hiyo mistari ya kontua zinaonyesha jinsi gani eneo linapanda juu au kutelemka. Kama mistari iko karibu sana mtelemko ni mkali; kama eneo linapanda polepole umbali baina ya mistari ya kimo tofauti ni kubwa zaidi. Pale ambapo mistari ya kontua inakutana mahali pamoja kuna mtelemko mkali wa ghafla.

Mistari ya kontua hutumiwa pia katika ramani za hali ya hewa zinazoonyesha maeneo yenye kanieneo tofauti au maeneo yenyo jotoridi tofauti.

Mifano ya matumizi ya kontua[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: