Kombora

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kombora
Kombora

Kombora ni neno linaloweza kutaja chochote kinachorushwa au kinachotupwa katika eneo lengwa. Siku hizi, inamaanisha hasa mfumo wa silaha unaojiongoza.

Makombora hutumiwa katika vita ili kuharibu malengo ya kijeshi. Makombora yanaweza kubeba mabomu au mizigo mingine yenye uharibifu. Mizigo ambayo kombora linaweza kubeba huweza kuitwa shehena (kwa Kiingereza Payloads).