Kombolela (tamthilia)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kombolela ni tamthilia ya televisheni kutoka nchini Tanzania. Imetayarishwa na Kisimani Films na kuongozwa na Majag Imeanza kurushwa hewani mwaka 2021 katika chaneli ya Sinema Zetu kwenye Azam TV kila Ijumaa hadi Jumapili saa moja jioni. 

Kombolela alishinda tuzo zaMajic vibe Awards kama mfululizo bora wa televisheni wa mwaka wa 2021[1].

Muhtasari[hariri | hariri chanzo]

Ustaarabu umezikwa, kazi hazionekani, pesa nazo zimejificha, wanakula kilichopo na wamejaa nyumba haipumui.

Maelezo ya jumla[hariri | hariri chanzo]

Kombolela ni tamthilia inayoelezea familia ya Mzee Kikala[2] ambayo ni familia ya Kiswahili iliyojaa visa, mikasa, upendo, vurugu, majungu na chuki. Wanafamilia wote huishi pamoja katika nyumba ya baba yao Mzee Kikala huku wakimtegemea kwa kila kitu.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Tuzo za filamu Tanzania 2022 vipengele 25 kuwaniwa (en). Mwananchi (2022-09-30). Jalada kutoka ya awali juu ya 2022-10-28. Iliwekwa mnamo 2022-10-29.
  2. Mzee Kikala: Nina watoto wengi kuliko wa kwenye Kombolela (en). Mwananchi (2022-05-01). Jalada kutoka ya awali juu ya 2022-10-28. Iliwekwa mnamo 2022-10-29.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kombolela (tamthilia) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.