Nenda kwa yaliyomo

Kizu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kizu
Kizu domo-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Accipitriformes (Ndege kama vipanga)
Familia: Accipitridae (Ndege walio na mnasaba na vipanga)
Nusufamilia: Melieraxinae
Jenasi: Melierax
Gray, 1840
Ngazi za chini

Spishi 4:

Vizu ni ndege mbuai wa jenasi Melierax, jenasi pekee ya nusufamilia Melieraxinae katika familia Accipitridae. Mgongo na mabawa yao ina rangi ya kijivu na tumbo lao ni mweupe na milia kijivu. Spishi zote zinatokea Afrika kusini kwa jangwa la Sahara. Zinapenda mahali pakavu kwenye miti. Hujenga tago lao kwa vijiti juu ya mti na hutaga mayai mawili au matatu, pengine yai moja. Wakati wa majira ya kuzaa huimba kwa milio ya mluzi. Hukamata wanyama na ndege wadogo na wadudu wakubwa.