Kipepesi
Kipepesi au mashine ya nukushi (kwa Kiingereza: fax machine) ni kifaa kinachotumika ili kutuma faksi, yaani nakala ya hati inayopatikana kwenye karatasi, kwa kipepesi kingine.
Ndani yake kuna sehemu mbili za skana (kisoma maandishi) na printa (sehemu ya kuchapisha). Skana inatafsiri uso wa karatasi kuwa alama za umeme zinazorushwa kupitia nyaya za simu hadi kipepesi kingine inayotafsiri tena alama za umeme kuwa amri kwa sehemu yake ya printa inayopuliza wino kwenye karatasi tupu, na hivyo kuunda nakala.
Tangu ufanyike usambazaji wa kompyuta kwenye ofisi pamoja na mashine za kuchapisha zenye skana, faksi hazitumiwi tena sana[1]. Kuna pia simu za mkononi nyingi zenye uwezo wa kupiga picha ya hati na kuituma kwa mpokeaji anayeweza kuchapisha picha aliyopokea sawa na faksi za zamani.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Kahigi, K. K. (2007). Ujanibishaji wa Office 2003 na Windows XP kwa Kiswahili Sanifu. Kioo cha Lugha, 5(1).
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |