Kangaja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kinuka (samaki))
Kangaja
Kangaja macho-mlia (Acanthurus dussumieri)
Kangaja macho-mlia (Acanthurus dussumieri)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Perciformes (Samaki kama ngege)
Familia: Acanthuridae (Samaki walio na nasaba na kangaja)
Bonaparte, 1832
Jenasi: Jenasi 3:
Spishi: Spishi za Afrika: 25

Kangaja au vinuka ni samaki wa baharini wa jenasi Acanthurus, Ctenochaetus na Prionurus katika familia Acanthuridae wa oda Perciformes ambao wana rangi kali na jozi ya miiba kwa umbo la vijembe, mmoja kwa kila upande wa msingi wa mkia. Spishi fulani huitwa kinanzua, kingoye, togoo au tongoo pia.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Sifa bainifu ya kangaja ni miiba kwa umbo la vijembe, mmoja au miwili kila upande wa mkia ("mikia ya miiba"), ambayo ni mikali na hatari sana na hutumiwa kama ulinzi uliokithiri. Kwa sababu hii, samaki hawa wana rangi kali za onyo. Pezimgongo na pezimkundu ni makubwa na yanaenea kwa kariba urefu wote wa mwili. Mdomo mdogo una safu moja ya meno yanayotumika kwa kujilisha na miani.

Kangaja wanaweza kujilisha peke yao, lakini mara nyingi husafiri na kujilisha pia katika makundi. Kujilisha katika makundi kunaweza kuwa njia ya kuzonga majibu makali ya ulinzi ya matima wadogo wa jitihada ambao wanajitahidi kulinda sehemu ndogo za miani kwenye miamba ya matumbawe.

Spishi nyingi ni ndogo na zina urefu hadi sm 15-40, lakini baadhi ya wanajenasi wa Acanthurus na Prionurus wanaweza kukua wakubwa zaidi. Samaki hawa wanaweza kukua haraka katika matangi-samaki, kwa hivyo lazima ukubwa wa wastani ukaguliwe na kama wanafaa kabla ya kuwaongeza katika tangi la samaki wa baharini.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kangaja kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.