Kimondo cha Chelyabinsk

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kimondo cha 2013 juu ya mkoa wa Chelyabinsk kilichora mstari wa moshi kwenye anga
Anguko na mlipuko wa kimondo cha Chelyabinsk
Uharibifu wa kiwanda mjini Chelyabinsk baada ya anguko la kimondo

Kimondo cha Chelyabinsk kilianguka tar. 13 Februari 2013 katika eneo la Chelyabinsk, Urusi mnamo saa tatu za asubuhi. [1]

Hiki kimondo kikubwa au asteroidi ndogo kilipasuka takriban 15 - 25 km juu ya uso wa dunia na nguvu ya mlipuko wake ilidhuru sehemu za nyumba na kusababisha zaidi ya watu 1200 kujeruhiwa. Vipande vya kimondo vilianguka chini bila taarifa za uharibifu wa mali au watu.

Gimba hili kutoka anga-nje lilikuwa kimondo au asteroidi ndogo ambalo halikutambuliwa mapema. Dakika 20 baada ya saa 3 asubuhi watu waliona mpira wa moto angani lililotoka upande wa mashariki ukielekea magharibi. Mpira wa moto ulikimbia ndani ya wingu la moshi lililochora mstari angani. Gimba hili liliwaka na kung'aa kushinda jua kwa muda mfupi. Nuru hii ilifuatwa na sauti kubwa na mshtuko uliovunja vyoo vya madirisha katika sehemu kubwa ya Chelyabinsk na mazingira yake. Watu wengi walijeruhiwa na vipande vya kioo. Nyumba kadhaa zilidhuriwa sehemu za paa au ukuta. Hakuna taarifa ya vifo. [2][3].

Makadirio ya kitaalamu[hariri | hariri chanzo]

Tofauti na asteroidi 2012 DA14 iliyopita Dunia karibu sana siku ileile kimondo cha Chelyabinsk hakikutazamiwa kabla kwa sababu mbili kwanza kwa sababu kilikuwa kidogo zaidi na pili kwa sababu njia yake ilitokea upande wa Jua na hivyo ilikuwa vigumu kuona.

Wataalamu walianza kufanya makadirio juu ya kimondo hiki kutokana na picha nyingi zilizochukuliwa wakati wa kupita juu ya Chelyabinsk na vipimo vilivyowezekana.

Kufuatana na taasisi ya Marekani NASA ukubwa wa gimba ulikuwa kipenyo cha mita 17 na masi yake baina tani 6 hadi 10. Kimondo hiki kilikuwa na mbio wa 54,000 km/h au kilomita 15 kwa sekunde. Imekadiriwa ya kwamba wakati wa kuchoma na kupasuka angani kiliachisha nishati iliyolingana na tani 500,000 za baruti ya TNT au takriban mara 20 - 30 kiasi cha nishati kilichoachishwa wakati wa mlipuko wa bomu la nyuklia wa Hiroshima.

Mshtuko wa mlipuko ulikuwa na nguvu kiasi ya kupimwa kwenye ardhi kama tetemeko dogo la ardhi.

Kulingana na nishati kubwa ya mlipuko huu uharibifu ulikuwa mdogo na sababu yake ni kwamba kimondo kilianza kuwaka katika angahewa na kupasuka wakati ilikuwa bado juu sana.

[4][5].

Tukio hili lilikuwa makumbusho ya hatari zinazoweza kutokea kwa magimba ya kukaribia dunia kutoka angani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Meteor in central Russia injures at least 500". USA Today. Iliwekwa mnamo 15 February 2013.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Major, Jason. "Meteor Blast Rocks Russia". Universe today. Iliwekwa mnamo 15 February 2013.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "500 injured by blasts as meteor falls in Russia". Yahoo News. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-02-18. Iliwekwa mnamo 15 February 2013.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. "Are 2012 DA14 and the Chelyabinsk meteor related?". FI: Sodankylä Geophysical Observatory. 15 February 2013. Iliwekwa mnamo 15 February 2013.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  5. "Russia Meteor Not Linked to Asteroid Flyby". NASA. 15 February 2013. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-02-17. Iliwekwa mnamo 15 February 2013.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
Wikimedia Commons ina media kuhusu: