Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kwa maana mengine tazama Kiluwiluwi
Viluwiluwi ni ndege wa familia ndogo Vanellinae katika familia Charadriidae . Spishi hizi ni kubwa kuliko zile za familia ndoga ya Charadriinae . Huonekana mara kwa mara kando ya maji, lakini spishi nyingi huonekana pia mbali na maji hata kwa maeneo makavu. Hutaga mayai yao chini na hula wadudu hasa.
Vanellus albiceps , Kiluwingozi Utosi-mweupe (White-headed au White-crowned Lapwing)
Vanellus armatus , Kiluwiluwi Fundichuma (Blacksmith Lapwing )
Vanellus coronatus , Kiluwitaji (Crowned Lapwing )
Vanellus crassirostris , Kiluwiluwi Madole-marefu (Long-toed Lapwing )
Vanellus gregarius , Kiluwiluwi Makundi (Sociable Lapwing )
Vanellus leucurus , Kiluwiluwi Mkia-mweupe (White-tailed Lapwing )
Vanellus lugubris , Kiluwijivu (Senegal au Lesser Black-winged Lapwing)
Vanellus melanocephalus , Kiluwiluwi Kidari-madoa (Spot-breasted Lapwing )
Vanellus melanopterus , Kiluwiluwi Mabawa-meusi (Black-winged Lapwing )
Vanellus senegallus , Kiluwingozi (African Wattled Lapwing )
Vanellus spinosus , Kiluwiluwi Kizibao-cheusi au Chekehua (Spur-winged Lapwing au Spur-winged Plover)
Vanellus superciliosus , Kiluwiluwi Kidari-chekundu (Brown-chested Lapwing )
Vanellus tectus , Kiluwiluwi Kishungi (Black-headed Lapwing )
Vanellus vanellus , Kiluwiluwi wa Ulaya (Northern Lapwing )
Kiluwiluwi kizibao-cheusi