Kilivvi-Kareli
Mandhari
Kilivvi-Kareli (pia Kiolonets) ni lugha ya Kiurali nchini Ufini na Urusi inayozungumzwa na Walivvi. Mwaka wa 2010 idadi ya wasemaji wa Kilivvi-Kareli nchini Urusi imehesabiwa kuwa watu 25,600. Pia kuna wasemaji 5170 nchini Ufini (2000). Idadi ya Walivvi ni zaidi ya laki mbili yaani kuna Walivvi wengi wanaotumia lugha za Kirusi au Kifini kama lugha ya kwanza badala ya lugha yao ya asili. Hata hivyo, kuna jitihada za kufufua na kuendeleza lugha ya Kilivvi-Kareli. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kilivvi-Kareli iko katika kundi la Kifini. Ingawa inafanana na Kikareli na Kifini, ni lugha tofauti. Pia ni tofauti na lugha za Kiludi na Kiveps. Wengine huangalia lugha hizo kuwa lahaja za Kikareli.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- lugha ya Kilivvi-Kareli kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kilivvi-Kareli Archived 14 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- lugha ya Kilivvi-Kareli katika Glottolog
- lugha ya Kilivvi-Kareli kwenye Ethnologue
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kilivvi-Kareli kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |