Kiludi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kiludi ni lugha ya Kiurali nchini Urusi inayozungumzwa na Waludi. Mwaka wa 2012 idadi ya wasemaji wa Kiludi imehesabiwa kuwa watu 3000. Waludi wengi wanaotumia lugha ya Kirusi, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Hata hivyo, nchini Ufini kuna jitihada za kufufua na kuendeleza lugha ya Kiludi.

Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiludi iko katika kundi la Kifini. Ingawa inafanana na Kilivvi na Kiveps, ni lugha tofauti. Wengine huangalia lugha hizo kuwa lahaja za Kikareli.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiludi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.