Kikazakhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kikazakh)
Eneo la uenezaji wa lugha ya Kikazakhi

Kikazakhi ni moja ya lugha za Kiturki za magharibi nchini Kazakhstan, Uchina, Uajemi, Mongolia, Uturuki na Uzbekistan inayozungumzwa na Wakazakh.

Kwa lugha yenyewe kuna majina "Қазақ Тілі (kasak tili), Қазақша (kazaksha) kwa mwandiko wa kikirili; Qazaq tili, Qazaqşa kwa mwandiko wa Kilatini, au قازاق ڌﻳل (kazak tili) kwa mwandiko wa Kiarabu.

Kikazakhi ni lugha rasmi katika nchi za Kazakhstan, Uchina na Urusi.

Wasemaji[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 2009 idadi ya wasemaji wa Kikazakh nchini Kazakhstan imehesabiwa kuwa watu karibu milioni kumi. Pia kuna wasemaji 1,250,000 nchini Uchina (2000), 500,000 nchini Urusi (2002), 992,000 nchini Uzbekistan (2010), 7700 nchini Uturuki (2014), 3000 nchini Uajemi (1982), na kuna Wakazakh 106,000 nchini Mongolia (2010) ambao wengi wao huongea Kimongolia ya Halh lakini.

Mwandiko[hariri | hariri chanzo]

Kihistoria Kikazakhi kiliwahi kuandikwa kwa herufi za asili ya Kiaramu. Katika karne zilizopita alfabeti za Kikirili, Kiarabu na Kilatini zilitumiwa.

Katika Kazakhstan na Mongolia lugha inandikwa kwa herufi za Kikirili. Huko China wasemaji wa kikazakhi hutumia alfabeti ya Kiarabu.

Mwaka 2006 serikali ilipeleka mapendekeazo ya kutumia herufi za Kilatini.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]