Kidaku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kidaku
Kidaku kusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Muscicapoidea (Ndege kama shore)
Familia: Muscicapidae (Ndege walio na mnasaba na shore)
Nusufamilia: Muscicapinae (Ndege wanaofanana na shore)
Jenasi: Dioptrornis Fischer & Reichenow, 1884

Melaenornis G.R. Gray, 1840

Vidaku ni ndege wadogo wa jenasi Dioptrornis na Melaenornis katika familia Muscicapidae. Spishi nyingine inaitwa chekiro. Ndege hawa wana rangi kijivu au nyeusi. Wanatokea misitu na maeneo mengine yenye miti katika Afrika. Hula wadudu. Kwa kawaida vidaku hukaa tawi wakiangalia ujirani. Wakiona mdudu huruka ili kumkamata na kurudi tawi. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika tundu la mti au dhidhi ya shina. Jike huyataga mayai 2-6.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]