Ketubimu
Mandhari
Ketubimu (כתובים, Ketuvim, wingi wa ketuv, ambalo ni sawa na Kiarabu/ Kiswahili "kitab/kitabu") ni sehemu ya tatu na ya mwisho ya Biblia ya Kiebrania (תנ״ך, Tanakh, kifupisho kinachounganisha herufi tatu "T" - "N" - "Kh" ambazo ni mianzo ya maneno matatu ya Kiebrania yanayotaja sehemu tatu ndani ya Biblia ya Kiebrania: Torati, Neviim, Ketuvim).
Vitabu hivi hugawanywa katika kundi za:
- vitabu vya kihistoria kama vile Ezra, Nehemiah na Mambo ya Nyakati.
- vitabu vya hekima kama vile Ayubu, Mhubiri na Mithali.
- vitabu vya kishairi kama vile Zaburi, Maombolezo na Wimbo Ulio Bora.
- vitabu vingine kama vile Ruthu, Estha na Danieli.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ketubimu kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |