Kayayei

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kayayei
Nchi Ghana
kikundi cha wanawake wa Kayayei wakiandamana kwenye Gwaride la Siku ya Uhuru wa Ghana 2020 huko Kumasi
kikundi cha wanawake wa Kayayei wakiandamana kwenye Gwaride la Siku ya Uhuru wa Ghana 2020 huko Kumasi

Kayayei (pia Kaya Yei) ni neno lenye asili ya nchi ya Ghana lenye maana ya mwanamke, kuli au mbeba mizigo. Wanawake wa aina hiyo wamekuwa na tabia ya kuhama kutoka vijijini kwenda mjini kwa lengo la kutafuta kazi[1]. Njia yao kuu ya ubebaji mizigo ni kutumia vichwa vyao.

Etimolojia[hariri | hariri chanzo]

Neno kayayei (umoja wake ni kaya yoo) ni mchanganyiko unaoundwa kutoka lugha mbili zinazozungumzwa nchini Ghana. Kaya ina maana ya "mzigo, mizigo[1] au bidhaa"[2] katika lugha ya Kihausa, na Yei inamaanisha "mwanamke au wanawake" katika lugha ya Ga.[1] Watu wa Kumasi huwaita wapagazi paa o paa.

Majukumu[hariri | hariri chanzo]

Kaya daima wamekuwa vibarua wa mikono. Wanasafirisha bidhaa kwenda na kutoka sokoni, hasa bidhaa za kilimo.[3] Kwa kawaida, Kaya hubeba mizigo yao katika sufuria kubwa iliyowekwa juu ya vichwa vyao, wakina mama hao huweka kitambaa kilichozingirishwa na kulowekwa kwenye maji ili kuzuia maumivu ya kubeba sufuria hizo kichwani.

Mazingira ya kazi[hariri | hariri chanzo]

Kaya Yei bado wanataabika katika masoko nchini Ghana hadi leo hii, mara nyingi wapo katika hali duni na kipato kidogo. Mara kwa mara, Kaya huletwa katika nyumba za watu binafsi kufanya kazi za nyumbani, ambapo kupata kipato kidogo zaidi. Kaya mara nyingi ni kazi zao ni za muda mfupi, na mara nyingi huafanya kazi bila kuzingatia usafi.Kimisingi hali zao za ki usafi na lishe pia ni duni sana.Katika miji mikubwa kama vile mji wa Accra na Kumasi, Kaya mara nyingi ni wahamiaji kutoka maeneo ya mbali ambao wamekuja mijini kutafuta matarajio ya maisha bora ya ajira.[1][2]

Mnamo Mei mwaka 2016, Waziri wa Jinsia, Watoto na Ulinzi wa Jamii Nana Oye Lithur alihakikisha kwamba zaidi ya kayayei 1,000 kutoka soko la Agbogbloshie na Mallam Atta huko Accra walisajiliwa kwenye Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Afya, ili kuwasaidia kupata huduma ya msingi ya afya.[4] Katika bajeti ya mwaka ya 2017, Waziri wa Fedha Ken Ofori-Atta aliruhusu kuondolewa kayayei kwenye kulipa ushuru wa soko kwa makusanyiko yao mbalimbali.[5][6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kayayei kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.