Justus von Liebig

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Justus von Liebig.

Justus Freiherr von Liebig (12 Mei 1803 - 18 Aprili 1873) alikuwa mkemia wa Ujerumani ambaye alitoa mchango mkubwa katika kemia ya kilimo na biolojia, na anachukuliwa kuwa mwanzilishi wa kemia hai (organic chemistry).

Kama profesa katika Chuo Kikuu cha Giessen, alipanga mbinu za mafunzo ya kisasa ya maabara, na kwa ubunifu ule, anaonekana kama mmoja wa walimu bora wa kemia wakati wote huko Ujerumani.

Liebig alianzisha mbinu mpya za uchambuzi wa vifaa vya kikaboni. Alionyesha kuwa, ili mimea ikue inahitaji maji, jua kaboni dioksidi, madini na nitrojeni. Aligundua kuwa nitrojeni ilikuwa kirutubisho muhimu cha mimea, na alitengeneza mbolea ya kwanza ya nitrojeni. Alielezea pia athari za virutubisho vingine kwenye mimea.

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Justus von Liebig kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.