Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu
Mandhari
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (kwa Kiarabu منظمة التعاون الإسلامي; kwa Kiingereza Organisation of Islamic Cooperation, kifupi OIC; kwa Kifaransa Organisation de la Coopération Islamique) ni muundo wa kimataifa ulioanzishwa mwaka 1969, ambao kwa sasa unaunganisha nchi 57, zenye wakazi zaidi ya bilioni 1.6 (2008).
Jumuiya hiyo inajitambulisha kama "sauti ya pamoja ya umma wa Kiislamu" na inafanya kazi ya "kutetea na kulinda masilahi ya ulimwengu wa Kiislamu kwa roho ya kustawisha amani na uelewano kati ya mataifa yote".
Lugha rasmi za OIC ni Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Ankerl, Guy Coexisting Contemporary Civilisations: Arabo-Muslim, Bharati, Chinese, and Western. Geneva, INUPress, 2000, ISBN|2-88155-004-5.
- Al-Huda, Qamar. "Organisation of the Islamic Conference." Encyclopedia of Islam and the Muslim World. Edited by Martin, Richard C. Macmillan Reference, 2004. vol. 1 p. 394, 20 April 2008.