Jumeirah Lake Towers

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Jumeirah Lake Towers

—— Jamii ya United Arab Emirates ——
Jumeirah Lake Towers

Flag of the United Arab Emirates.svg

Nchi United Arab Emirates
Emirate Dubai
Mji Dubai
Takwimu za Jamii
Ukubwa 1.8 km²
Majamii Jirani Jumeirah Islands, Dubai Marina, Emirates Hills
Stesheni ya Reli ya Dubai Metro       Jumeirah Lake Towers 
Maandishi ya chini
Jamii hii bado linaendelea

Jumeirah Ziwa Towers (Kiarabu:|ابراج بحيرة الجميرا) ni eneo kubwa la maendeleo Dubai, United Arab Emirates ambalo lina majumba 79 yanayojengwa kando maziwa manne ya binadamu (Ziwa Almas Magharibi, Ziwa Almas Mashariki, Ziwa Elucio, na Ziwa Allure) vile vile, kuna jumba la JLT la 8 linalokabili visiwa vya Jumeirah. Maziwa haya (ambazo ni mita 3 kwenda chini) zitakuwa kzimejazwa kabisa mwisho wa 2009. [1] Jumla ya eneo lililofunikwa na maziwa, manjia ya maji na ardhi itakuwa mita miraba 730,000. Majumba yatakuwa na maghorofa mbalimbali, kutoka 35 hadi 45, isipokuwa lile la kati ambali litakuwa na ghorofa 66. Jumba refu kabisa na lile maarufu kabisa katika eneo hili litakuwa Almas Tower ambalo litakuwa katika kisiwa chake pekee kati ya Ziwa Almas Magharibi na Ziwa Almas Mashariki. Majumba yote ya makazi yatakuwa katika makundi ya tatu. Hili litarahisisha usambazaji wa barua.

Ukamilishaji wa Saba Tower mwezi Desemba 2006 uliadhimisha jumba la kwanza kukamilika katika Jumeirah Lake Towers. Jumba la mwisho linatarajiwa kukamilika mwaka 2011. Ujenzi mwingi utafanyika mwaka 2008.

Mwezi Oktoba 2008 jumla ya majumba 19 zilikuwa tayari kutumika na mengine 6 yanatarajiwa mwisho wa 2008.

Moto[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 18 Januari 2007, wafanyakazi wawili waliuawa na angalau 40 (wanne vibaya) kujeruhiwa wakati moto ulizuka katika ujenzi chini Fortune Tower. [2] Ujenzi wa Fortune Tower ulisimamishwa kwa miezi kadhaa, lakini unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa 2007.

Vichala[hariri | hariri chanzo]

Majumba katika JLT yamepangwa katika makundi 26, kila na majumba tatu, na yamepewa majina kutoka A hadi Z, kila nguzo kina eneo lake la maegesho na duka la rejareja. Majumba nayo yana majina 1, 2, 3 lakini pia yana majina rasmi. Vichala havina majina rasmi.

Hoteli[hariri | hariri chanzo]

Hoteli nne zitajengwa katika mradi, Mövenpick Hotel katika kiwanja A2, Bonnington Jumeirah Lakes Towers katika kiwanja J3, na hoteli zisizojulikana katika viwanja T3 na z2; kutakuwa pia na majumba ya makazi ya ghorofa.

Al Mas na Biashara ya Madini[hariri | hariri chanzo]

Jumba kuu ni jengo la Al Mas (Kiarabu: "ya Diamond") na hili ni makao kuu ya DMCC na pia Dubai Diamond Exchange. Wamiliki na wapangaji wote ni mafanyibiashara wa almasi. Upande wa chini wa jumba hili ndipo hifadhi ya almasi iko.

Majumba mengine yanayomilikiwa na DMCC, Au na Ag, yatakuwa makazi ya Dubai Gold Exchange na Dubai Silver Exchange mfululizo na pia litakuwa na wanachama wa DMCC pekee.

Idadi ya Watu na Vifaa[hariri | hariri chanzo]

Mradi huu unakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 60,000 na wanaokuja kufanya kazi 120.000; itakuwa na nyanja 5 za kuchezea za watoto, misikiti 3, kituo cha polisi, kituo cha ulinzi wa kiraia na vifaa vingine.

Kutakuwa na vituo viwili vya reli vya Dubai Light Rail na basi kutoka vichala kwa vituo hivi vya Reli zimepangiwa.

Hifadhi ya Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [2] ^ Ukweli wa Jumeirah Lake Towers
  2. [3] ^ Wafanyakazi kufa katika moto wa jumba la Dubai - BBC News - zilizopatikana tarehe 18 Januari 2007.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]