Dubai Marina
Dubai Marina
—— Jamii ya United Arab Emirates —— | |
Dubai Marina | |
Nchi | United Arab Emirates |
Emirate | Dubai |
Mji | Dubai |
Takwimu za Jamii | |
Ukubwa | 4.9 million m² |
Majamii Jirani | Al Sufouh, Emirates Hills, Palm Jumeirah |
Stesheni ya Reli ya Dubai Metro | Dubai Marina |
Nambari za Uratibu | 25°4′52.86″N 55°8′38.67″E / 25.0813500°N 55.1440750°E |
Dubai Marina ni eneo lililo mjini Dubai, ambao sasa unaitwa 'new Dubai'. Iko kwenye Interchange 5 karibu na Dubai Internet City na Dubai Media City. Upande mmoja wa eneo hili limemalizika kujengwa. Dubai Marina limebuniwa na kujengwa kama Concord Pacific Place iliyo kwenye False Creek mjini Vancouver, BC, nchini Canada.[1]
'Marina' yote imejengwa na kampuni ya ujenzi ya Emaar Properties iliyopo mjini Dubai. Sehemu ya kwanza ya Dubai Marina ipo kwenye ardhi ya eka 25 - ambapo kuna ghorofa sita za nyumba (Dubai Marina Towers) na majumba 64 ya anasa zilizo na mabustani kwenye dari zao. Ghorofa tatu kati ya hizo zimepewa majina kutokana na almasi: Al Mass, Fairooz na Murjan na ghorofa zingine tatu zimeitwa majina ya manukato ya Kiarabu: Mesk, Anbar na Al Yass.
Sehemu ya pili ya Dubai Marina ina takriban ghorofa 200 zikiwemo Al Majeera Towers na Al Sahab twin towers. Marina nyingine iliyojengwa duniani ni Marina del Rey mjini California, Marekani.
Ghorofa ndefu kabisa ni kama Pentominium, Ocean Heights, Damac Heights, Princess Tower, Marina 101, Marina 106, Elite Residence, na 23 Marina.
Hifadhi ya picha
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "BCBusiness: False Creek, Dubai". bcbusinessonline.ca. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-06-29. Iliwekwa mnamo 2009-02-21.